Wednesday 16 January 2013

VIJIMAMBO: DIWANI AFUMANIWA UGONI IRINGA ACHEZEA KIPIGO

VIJIMAMBO
thumbnail DIWANI AFUMANIWA UGONI IRINGA ACHEZEA KIPIGO
Jan 16th 2013, 21:05


Katika hali isiyo  kuwa ya kawaida  diwani  mmoja wa chama  cha siasa jina laka  na chama  chake   limewekwa  kapuni  kwa   sasa amefumaniwa akivunja amri ya  sita  na mke  wa  mtu usiku  wa  leo na  kuchezea kichapo .

Diwani  huyo mpenda ngono anadaiwa  kufumaniwa  akiwa katika nyumba ya mpiga kura  wake huyo katika  kata     moja ya wilaya ya Iringa Vijijini na  ni diwani anayetokea katika wilaya ya Iringa mkoa  wa Iringa na ni diwani mtanashati kweli  kweli.

Mashuhuda  wa tukio  hilo  wameudokeza  mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com   kuwa  kutokana na fumanizi hilo la mwaka wapiga  kura  wake wanaoishi jirani na nyumba hiyo ambayo mheshimiwa alifunaniwa waliizunguka nyumba hiyo na  kuanza kumshikisha adabu  mheshimiwa  huyo.

Baada ya mheshimiwa  huyo  kuchezea kipigo  kutoka kwa  njema lenye mke  huyo pamoja na  wananchi alilazimika  kutoka mbio na kukimbilia porini kabla ya  kwenda  kupatiwa matibabu katika moja kati ya  zahanati  mbili  zilizopo katika  eneo hilo ikiwemo ya Misheni na ile ya  Kijiji  .

Iwapo  wataka  kujua zaidi  juu ya  tukio  hili  endelea  kufuatilia mtandao huu unapofanya  jitihada za  kumtafuta   diwani huyo

Pichani ni moja kati ya  picha ya  fumanizi ambayo inafanana  na fumanizi  hili la diwani japo hainamahusiano na tukio  hili

KWA HISANI YA HABARI ZA JAMII BLOG

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment