Saturday 19 January 2013

VIJIMAMBO: MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR ZBC WAFUNGULIWA

VIJIMAMBO
thumbnail MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR ZBC WAFUNGULIWA
Jan 19th 2013, 21:20

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui,(katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Juliun Raphael,alipowasili katika Viwanja vya Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,kuufungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,(kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahaya Mzee,na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui.
Wadau wa Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara ZBC wakiwa katika Mkutano Uliofanyika kwa kujadili masuala mbali mbali ya kukuza Uchumi wa Taifa ,Mkutano huo ulifanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.
Wajumbe wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar,kutoka Taasisi na Makampuni mbali mbali ,wakifuatilia kwa makini taarifa na mada zilizotolewa katika mkutano huo,uliofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel,Mjini Unguja.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisikiliza kwa makini mada mbali mbali zilizotolewa katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Baadhi ya watendaji wa Taasisi mbali mbali wakifuatilia kwa makini agenda za mkutano wa Saba ( 7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.)

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment