Monday 21 January 2013

VIJIMAMBO: WAASISI WA MUUNGANO WATOA MAONI YAO

VIJIMAMBO
WAASISI WA MUUNGANO WATOA MAONI YAO
Jan 22nd 2013, 00:05


Salum Rashid                          Nassor Hassan Moyo

Na Salma Said, Zanzibar

WANASIASA wakongwe waliokuwa katika serikali wakati wa kuundwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Salum Rashid na Nassor Hassan Moyo wamesema baraza la Mapinduzi halikushauriwa wala halikushirikishwa katika kuundwa kwa Muungano huo.

Hayo wameyasema mbele ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya wanasiasa hao kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba huko Maisara Mjini Unguja.

Wanasiasa hao wameieleza tume kwamba tokea awali ya kuundwa wa Muungano huo ulikosekana uhaliali wake pamoja na kwamba umedumu kwa miaka hamsini lakini kulikuw ana malalamiko hayo.

Hata hivyo wanasiasa wote wawili wameunga mkono kuwepo kwa Muungano wakisema ni jambo muhimu lakini wakitaka kuwepo na mfumo mpya na muundo wake ambapo wote wamekubaliana kuwepo kwa Muungano wa Mkataba.

Wote wawili walisema kwa hali ilivyotokea miaka hamsini wa muundo wa Muungano kushindwa kutatua mambo mbali mbali mfumo pekee unaofaa kwa sasa na kwa kizazi hiki ni ule mfumo wa Muungano wa mkataba ambapo walisema utaratibu wake utajulikana baadae.

Mzee Moyo aliwahi kuwa Waziri wa kwanza wa Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Salum Rashid alikuwa katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar wamesisitiza kuendelea kuwepo kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku wakitaka muundo mpya utakaoimarisha Muungano huo kuwa na tija zaidi kwa pande mbili ni kusikilizwa kwa maoni ya wananchi ambao wanataka muungano wa Mkataba.

Mzee Moyo alisema serikali isiogope maoni ya wananchi kwani kwa takriban miaka 50 matatizo ya Muungano yameshindwa kutatuliwa na njia pekee kwa sasa ni kukubali kubadilisha mfumo amabo utakwenda sambamba na wakati huu ambapo idadi kubwa ya wananchi wameamka na kuona kwamba kuna tatizo katika Muungano uliopo.

"Sisi ndio tulikuwa na dhamana wakati ule na tulitakiwa tuunganishe serikali kwa kuimarisha udugu na kuimarisha uchumi wetu lakini bahati mbaya sasa tena kumekuwepo na kero lakini mimi siziiti kero naita ni matatizo kwa hivyo haya matatizo ni wakati wake kuondoshwa" alisema Mzee Moyo.

"Mimi msimamo wangu mimi ni serikali ya mkataba na ndio ninavyoamini na mimi naamini kwamba huu muungano tulinao ni mkataba na hili sio jambo jipya si Mwalimu Nyerere na Mzee Karume alitia mkataba, hili sio jambo jipya" alisema Mzee Moyo.

Hata hivyo alisema muundo wa Muungano uliopo sasa unahitaji marekebisho makubwa kwani unaonekana upande mmoja kushindwa kufaidika na fursa za Muungano ziliopo sasa na hivyo kuibuwa malalamiko miongni mwa wananchi.

Mzee Moyo alitaka kurudishwa kwa utaratibu wa zamani ambapo rais wa Zanzibar anakuwa makamo wa kwanza wa rais wa Muungano, kwani nchi zinazounda Muungano huo ni Tanganyika na Zanzibar na hivyo Rais kutokuwa makamo amenyimwa mamlaka yake.

"Malalamiko makubwa ya wananchi wa Zanzibar ni kuwa rais wa Zanzibar sasa sio makamo wa kwanza wa rais wa Muungano, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaundwa na nchi mbili ya Zanzibar na Tanganyika sasa inakuwaje rais wa Zanzibar sio tena sehemu ya Muungano huo, hii ni kinyume na makubaliano ya Muungano" alisema.

Alisema kitendo cha kuondowa nafasi ya rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa kwanza wa muungano kwa kiasi kikubwa kimedhoofisha Muungano na kuifanya Zanzibar kushindwa kufaidika na fursa nyingi za Muungano na kuibuka kwa kasoro nyingi ambazo zinajulikana kwa jina la kero ambapo yeye alisema sio kero bali ni matatizo makubwa ndnai ya Muungano huo.

Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar ambaye alishuhudia makubaliano ya Muungano wakati alipokwenda DAR ES salaam yeye na Mzee Karume siku ya kutiwa saini kwa Mwalimu Nyerere, Mzee Salum Rashid alisisitiza kuendelea kuwepo kwa Muungano wa pande mbili lakini ule utakaokuwa na maslahi na faida kwa wananchi wa pande mbili hizo.

Akitoa maoni yake Mzee Rashid alisema serikali isiwe na woga kwani kuvunjika kwa Muungano sio jambo kubwa na wala sio geni kwani baadhi ya nchi za Afrika zimeshawahi kuungana na Muungano huo ukavunjika.

"Mimi sioni jambo zito kuvunja Muungano mbona Muungano wa Senegal na Gambia umevunjika na wote walikuwa ni wanachama wa Umoja wa Afrika na hakuna jambo lolote lililotokea, lakini sisi tunaotaka Muungano wa Mkataba hatusemi tuvunje Muungano au Muungano usiwepo la hasha sisi tunataka mfumo mpya wa Muungano ambao utaipa mamlaka na madakra Zanzibar ya kujihudumia ili iondoshe kasoro iliyopo ambayo Zanzibar ipo lakini haina mamlaka" alisema Mzee Rashid.

Alisema kuwepo nje ya serikali sio sababu ya kuwa wao ndio wana fursa ya kuonge ahayo lakini wakati ule ukiongea suala la Muungano ilikuwa unaonekana ni haioni.

"Tulikuwa tunataka kuongea lakini kwa wakati ule hungeweza kuonge alolote kwa sababu ukisema suala lolote la Muungano ulikuwa unaonekana wewe haini na sheria ya haina unauliwa sasa nani angethubutu kuongea suala hilo" alisema.

Alisema kwa sasa haiwezekani tena kuburuzwa watu hasa vijana hivyo matumaini yake kwa tume ya Jaji Warioba ni makubwa kwamba watafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa na kuleta yape mapendekezo ambayo wananchi wameyatoa katika mkusanyaji wa maoni ya katiba.

Alisema Muungano wa Mkataba ndio sahihi kwa sasa na hakuna sabbau ya kuogopa hilo kwani wananchi hasa vijana wamekuwa wanataka kuona nchi yao ikiwa na mamlaka kamili pamoja na rais wao kuwa na hadhi kama rais.

"Muungano wa mwanzo haaukushauri wala kushirikishwa wananchi wa Zanzibar kuhusu Muungano wa nchi yao kwa hivyo Muungano huu wa miaka hamsini lakini sasa unahitaji kuwa na mfumo mpya wa Muungano" alisema Rashid.

Mzee Rashid alipendekeza kuwepo kwa kipindi cha mpito iwapo utavunjwa Muungano kutakuwa na Muungano wa kudumu wa utawala na pande mbili hizo zitapata kupanga namna gani ya kuweka mkataba kati ya pande mbili hizo.

Mzee Moyo na Mzee Rashid wote wawili wamewataka wananchi kutokuwa na khofu na tume hiyo wakisema wao binfasi wanaimini kwamba itafanya akzi zake kwa uadilifu hasa kwa kuzingatia maoni yaliotolewa na wananchi wa pande mbili hizo yamezingatiwa na kufanyiwa kazi.

Aidha walifurahishwa na utaratibu wa sasa wa kuwashirikisha waasisi na watu mashuhuri katika kutoa maoni ya katiba mpya na kusema hatua hiyo inaonesha kupanuka kwa demokrasia nchini na uhuru wa watu kutoa maoni jambo ambalo huko nyuma halikuwepo na utaratibu uliokuwa ukitumika ni ule viongozi kuwaamulia wananchi

"Nashukuru sana kushirikishwa katika masuala ya katiba ya Muungano.....Zamani ukizungumza mambo yanayohusu Muungano unaonekana wewe ni sawa na mhaini ambaye hukumu yake ni kunyongwa lakini sasa afadhali bwana, alisema Mzee Rashid na kuongeza kuwa anaamini tume itafanya kazi vyema.

Na Mzee Moyo alisema matumaini yake makubwa kwamba tume iliyopewa jukumu hilo itatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba kwani inaundwa na wajumbe wenye uwezo ambao baadhi yake wameshika nyadhifa kubwa nchini na hivyo wananchi wasiwe na khofu na tume hiyo kwa kuwa katua za awali imefanya vizuri.

Tume ya kukusanya maoni ya katiba ikiongozwa na mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Joseph Warioba na Makamo wake Assa Rashid iliendelea na kazi yake ya kukusanya maoni ya katiba kutoka kwa makundi maalumu ikiwemo viongozi wakuu ambapo tayari waliokwisha kutoa maoni yao ni pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Rais Mstaafu Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume na baadhi ya waasisi wa Mapinduzi.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment