Tuesday 22 January 2013

VIJIMAMBO: WAZIRI SAMWEL SITTA, DKT MBUKI FELESHI NA MTANDAO WA KINGA JAMII WATOA MAONI YAO KUHUSU KATIBA MPYA

VIJIMAMBO
thumbnail WAZIRI SAMWEL SITTA, DKT MBUKI FELESHI NA MTANDAO WA KINGA JAMII WATOA MAONI YAO KUHUSU KATIBA MPYA
Jan 22nd 2013, 20:56

Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Mabadiliko ya Katiba jana (Jumatatu Januari 21, 2013) jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju na Wajumbe wa Tume Bw. Humphery Polepole na Bw. Awadhi Said.

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana (Jumatatu Januari 21, 2013). Kushoto ni Mjumbe wa Tume Bi. Maria Kashonda.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta (katikati) akiagana na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) na Bw. Nassoro Mohammed (kulia) mara baada kiongozi huyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana.
Mjumbe wa Mtandao wa Kinga Jamii (TPSN - Tanzania Social Protection Network) Bi. Clotilda Isdor akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko uliofanyika jana (Jumatatu Janauari, 21, 2013). Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Tume, Bi. Mwatumu Malale.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Mohammed Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya kitengo cha utafiti cha Tume kwa ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) ulioongozwa na Makamishina wa Tume hiyo, Jaji Ernest Mwipopo (wa tatu kulia) na Bi. Esther Manyesha (wa nne kulia). LRCT imewasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya kwa Tume jana.
Kamishina wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT), Jaji Ernest Mwipopo akikabidhi maoni ya LRCT hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana (Jumatatu Januari 21, 2013). Katikani ni Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohammed.
(Picha na Tume ya Mabadiliko ya Katiba)

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment