Monday 24 December 2012

VIJIMAMBO: MAALIM SEIF AKUTANA NA MABALOZI WA INDIA NA MSUMBIJI

VIJIMAMBO
thumbnail MAALIM SEIF AKUTANA NA MABALOZI WA INDIA NA MSUMBIJI
Dec 25th 2012, 00:02

Balozi mdogo wa India aliyepo Zanzibar Pawan Kumar akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ofisini kwake Migombani.
Balozi mdogo wa India aliyepo Zanzibar Pawan Kumar akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ofisini kwake Migombani. Kushoto ni ofisa wa ubalozi wa India bwana Rao.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi kitabu cha urithi wa Zanzibar balozi mdogo wa India Pawan Kumar baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na balozi mdogo wa India Pawan Kumar baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.
Balozi mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar Bw. Benuardo Constatino Lidimba akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na balozi mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar Bw. Benuardo Constatino Lidimba ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na balozi mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar Bw. Benuardo Constatino Lidimba baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.

ZANZIBAR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali inathamini sana mchango unaotolewa na serikali ya India katika kukuza uchumi na ustawi wa wananchi wa Zanzibar.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo alipokuwa na mazungumzo na balozi mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bw. Pawan Kumar huko ofisini kwake Migombani.
Amesema India imeendelea kuwa mshirika wa karibu wa Zanzibar katika kusaidia maendeleo ya nchi hasa katika sekta za Afya na elimu.
Amefahamisha kuwa Zanzibar imekuwa ikinufaika kikamilifu kutokana na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati yake na India, na kusisitiza kuendelezwa kwa ushirikiano huo kwa maslahi ya pande hizo mbili.
Amesifu umakini wa watumishi wa India hasa katika sekta ya afya, sambamba na kusifu ubora wa elimu inayotolewa nchini humo, na kwamba Zanzibar inaweza kujifunza zaidi katika maeneo hayo.
Kwa upande wake balozi mdogo wa India Bw. Pawan amemuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika maeneo tofauti yakiwemo kutoa fursa za masomo kwa wanafunzi wa Zanzibar.

Amefahamisha kuwa idadi ya wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma nchini India imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka huu wa masomo jumla ya wanafunzi 72 wamepatiwa fursa hiyo tofauti na mwaka jana ambapo walikuwa wanafunzi 48.
Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amekutana na balozi mdogo wa Msumbiji Bw. Benuardo Constatino Lidimba aliyefika ofini kwake kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wa utumishi hapa nchini.

Katika mazungumzo hayo balozi Lidimba ameishauri Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar kuangalia uwezekano wa kukuza biashara kati ya Zanzibar na Msumbiji, kwa kuwawezesha wafanyabiashara kuweza kufanya shughuli zao za uhakika.
Amesema wafanyabiashara wengi wa Zanzibar wanaofanya biashara nchini Msumbiji wamekuwa wakibahatisha maisha yao kutokana na kutumia usafiri wa majahazi ambao sio wa uhakika kuweza kufanyia shughuli hizo.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais amesema serikali inaendelea kulifanyia kazi tatizo hilo ambapo kwa sasa imo katika mkakati wa kutafuta meli mpya kwa ajili ya kupata usafiri wa uhakika, utakaowawezesha wananchi na wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa uhakika.
Amesema katika kukabiliana na tatizo hilo serikali pia imekuwa ikifanya mazungumzo na wafanyabiashara mbali mbai ili waweze kuwekeza katika sekta ya usafiri wa baharini.
Ameongeza kuwa lengo la serikali ni kuwa na usafiri wa kisasa na wa uhakika ambao utasaidia kuiunganisha Zanzibar na nchi jirani, hatua ambayo itasaidia kukuza uchumi kwa haraka.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment