Tuesday, 26 February 2013

VIJIMAMBO: Rais Kikwete akagua Ukumbi mpya Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar

VIJIMAMBO
thumbnail Rais Kikwete akagua Ukumbi mpya Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar
Feb 27th 2013, 04:21



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi mkubwa wa mikutano wa Julius Nyerere multi-purpose International conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali. Picha na Freddy Maro.
Sehemu ya jukwaa kuu
Nafasi za wajumbe wa mikutano
Viti
Upande wa juu

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment