Waziri wa Nishati na Madini Mh. Sospeter Muhongo alipata fursa kuongea na Watanzania waishio Uingereza katika mwaliko rasmi kutoka serikali ya Uingerza. Katika ziara yake nchini Uingereza Mh Sospeter Muhongo ameambatana na Bw. Athanas Macheyeki, Bw. Seleman Hatibu na Bw. Sosthenes Massola.
Mh. Muhongo aliwaeleza Watanzani suala zima la gas na jinsi gani serikali itavyotumia gas hiyo kuleta maendeleo ya nchi. Amesema "serikali itahakikisha kuwa kila kijiji kinapata umeme na mpaka kufikia mwaka 2025 nchi ya Tanzania itaondoka na umasikini". Aliendelea kusema kuwa bila ya umeme hatutoweza kutoa umasikini hivyo wizara yake itatafuta miundo mbinu ya kisasa ili kuwezesha suala zima la matatizo ya umeme linaondoka. Pia amesema wizara yake itaangalia tena ufumo wa Tanesco na kuanzisha idara zingine ambazo zitashirikiana na zitawezesha kutatua matatizo yanayoikabili Tanesco.
Vilevile Mh Muhongo aliwataka wawekezaji wa Kitanzania waweze kuwekeza katika sekta ya nishati na madini.
Habari na Ally Muhdin- London
Mh. Peter Kallaghe akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Sosper Muhongo kuongea na watanzania
Mama Balozi Joyce Kallaghe pia alikuwepo
Naibu Balozi Chabaka Kilumanga na watanzania waliohuduria wakifuatilia mkutano kwa makini
Wadau mbali mbali waliohudhuria mkutano huo wakisikiliza kwa makini
kwa picha zaidi bofya read more
Meya wa London Haruna Mbeyu (kushoto) na Mwenyekiti wa Watanzania London Said Surur (kulia) wakifuatilia mkutano
Kutoka kushoto Freddy Macha, mdau na Ma Nelly
Mkutano ukiendelea
Hussein Kova nae alikuwepo
Mdau akiuuliza swali
Katibu wa CCM UK Bi Mariam Mungula (kulia) akisikiliza kwa makini
Frank Eyembe wa Urban Pulse akiwa kikazi zaidi
Eddie nae alikuwepo
Waziri Muhongo akifafanua jambo huku Balozi Kallaghe akisikiliza kwa makini
Maswali yakiendelea
Mariam Mungula akimwaga sera zake
Waziri Muhongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa CCM London Bi Mariam Mungula pamoja na Meya wetu Haruna Mbeyu
Said Surur (kulia) na wadau wakiwakilisha ipasavyo
Minah, Hussein Kova pamoja na wadu wengine katika picha ya pamoja na Mh. Waziri
Mh. Balozi Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakina dada wakitanzania walio hudhuria mkutano huo
Mariam Mungula akiwa katika picha ya pamoja na Mh. Balozi Peter Kallaghe na Naibu Balozi Chabaka Kilumanga
Mh. Muhongo akiteta jambo na mdau Eli
Mdau Eddy katika picha ya pamoja na Mh. Muhongo
Ally Muhdin katika picha ya pamoja na Mh. Balozi
(picha kwa hisani ya JG Blog)
No comments:
Post a Comment