Wednesday, 2 January 2013

VIJIMAMBO: YALIYOMKUTA DIAMOND CLUB MAISHA NDIO HAYA!

VIJIMAMBO
thumbnail YALIYOMKUTA DIAMOND CLUB MAISHA NDIO HAYA!
Jan 2nd 2013, 19:20


VURUGU za makusudi zilizokuwa zimelenga kuharibu onyesho la msanii Naseeb Abdul "Diamond" jana usiku katika ukumbi wa New Club Maisha, zilikwama.

Watu kadhaa wanaominika kuwa wanatoka kwenye kambi ya msanii mmoja mpinzani wa Diamond, walikuwa wakimtukana na kumzomea Diamond na kutishia amani ndani ya ukumbi huo.

Watu hao waliendelea kufanya vurugu na kutupa chupa za maji jukwaani hali iliyopelekea wapenzi wa Diamond kuanza kujibu mapigo ghafla ukumbi ukawa uwanja wa vita, zikaanza kurushwa chupa za bia, viti na mambo mengine yaliyotishia amani hadi pale walinzi wa ukumbi huo walipofanikiwa kuwatoa nje na onyesho likaendelea.

Mara kadhaa Diamond alizima muziki na kusema: Mimi nimezaliwa mjini, kuna watoto wa Kariakoo nawaona hapa wanafanya fujo, najua wametumwa, hebu na nyie wazomeeni kidogo.

Ukumbi mzima ulipokea agizo la Diamond na kupiga mayowe ya kuzomea, hali iliyozidi kuchochea hasira za mashabiki wachache waliokuwa hawamkubali msanii huyo.Katika onyesho hilo, wasanii wengine wote walitumbuiza jana wakiwemo Ben Pol na Dully Sykes, walimaliza show zao salama bila vikwazo vyovyote lakini hali ilibadilika pale alipopanda Diamond na kupokewa na kelele za kejeli zilizojaa matusi ya nguoni.

Ukiachana na hali hiyo, Diamond kama kawaida yake alipiga bonge la show huku wimbo wake mpya "Kesho" ukirudiwa mara tatu kutokana na maombi ya mashabiki wengi.
Umati mkubwa ulifurika ukumbini hapo na hali ilikuwa ngumu kwenye foleni ya kukata tiketi.

Diamond aliiambia Saluti5 kwa njia ya simu kuwa kilichofanyika jana ni njama za watu waliozoea kupiga show za bure, lakini njama zao zimeshindwa na wataendelea kushindwa.

Msanii huyo amesema tayari kesi ipo polisi, watu waliofanya vurugu watakamatwa mmoja baada ya mwingine kwa vile wanajulikana na camera pia zilifanya kazi yake.


SOURCE:SALUTI 5

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment