Na Salma Said, Zanzibar
Serikali ya zanzibar imeombwa kuwasaidia wajane na mayatima kisiwani Pemba ambao wanakabiliwa na matatizo mengi ya kimaisha.
Ombi hilo liliwasilishwa jana katika kikao cha baraza la wawakilishi linaloendelea mjini hapa na mwakishi wa viti maalum vya wanawake (CUF) Mwanajuma Faki Mdachi ambaye alimtaka waziri kukutana na jumuia mpya ya wajane na watoto yatima pemba.
Akijadili ripoti ya utekelezaji wa kazi katika wizara ya Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wanawake na watoto kwa mwaka 2012/2013, Mwanajuwa alisema alisema wajane wanahitaji kusaidiwa ili kuondokana na ombaomba na kuishi maisha ya kubabaisha.
"Namuomba Waziri awatambuwe wajane kupitia jumuia yao kwa kukutana nao ili kuwasikiliza. Ni lazima wajane na yatima wasaidiwe," alisema Mwanajuma.
Naye Mwakilishi wa viti maalum vya wanawake (CCM) Asha Bakari Makame, alilalamikiwa kuongeza kwa udhalilishaji wa wananwake na watoto Unguja na pemba.
"Udhalilishaji na hasa ukabaji bado ni tatizo kubwa, ni lazima serikali ifanye juhudi za kudhibiti ili kuwalinda wanawake na watoto," alisema Asha huku akiungwa mkono na wajumbe wengine wa baraza hilo.
Akijibu hoja za wajumbe hao, waziri wa Ustawi wa jamii na maendeleo ya vijana, wanawake, na watoto Zainab Omar Mohammed aliwataka Wajumbe kuungana na serikali katika vita dhidi ya udhalilishaji.
"Vitendo vya udahlilishaji vimekithiri sana, lakini tunahitaji ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kushinda. Serikali pekee haiwezi, na nawaomba wananchi wasione aibu kutoa taarifa na kuja kutoa ushahidi mahakamani," alisema Zainab.
Waziri alisema kuwa tabia ya baadhi ya wananchi kuficha taarifa za ubakaji na kuogopa kutoa ushahidi mahakami inazorotesha juhudi za kupambana na uhalifu huo nchini, na kushauri elimu zaidi kwa wananchi
No comments:
Post a Comment