Monday, 24 December 2012

VIJIMAMBO: MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMTEMBELEA MZEE SAID NOOR ABDULKADIR NA KUTEMBELEA KITUO CHA MAFUNZO YA KOMPYUTA CHA CHWAKA, MKOA KUSINI UNGUJA LEO.

VIJIMAMBO
thumbnail MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMTEMBELEA MZEE SAID NOOR ABDULKADIR NA KUTEMBELEA KITUO CHA MAFUNZO YA KOMPYUTA CHA CHWAKA, MKOA KUSINI UNGUJA LEO.
Dec 24th 2012, 23:06

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakimsalimia Mzee Said Noor Abdulkadir, wakati alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake, Tunduni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, jana Desemba 23, 2012. Mzee huyo anasumbuliwa na maradhi ya mguu kwa muda wa miaka 13.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka na wananchi wa kijiji hicho, wakati alipofika katika kituo hicho leo Desemba 24, 2012 kwa ajili ya kujionea maendeleo ya kituo hicho, akiwa ameongozana na mkewe Mama Asha Bilal.
Sehemu ya Kompyuta zilizopo katika Kituo hicho cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka, Hamis Himid Ramadhan, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea ramani ya ujenzi mpya wa shule ya Chwaka, kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Fadhili Hamada Mshamba, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakiondoka katika Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya kituo hicho leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakizungumza na Mzee Silima Jendele, wakati Makamu alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Wazee leo, katika Mkoa wa Kusini Unguja.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment