Saturday 5 January 2013

VIJIMAMBO: JK kuwasili Singida kwa ziara ya siku mbili

VIJIMAMBO
thumbnail JK kuwasili Singida kwa ziara ya siku mbili
Jan 6th 2013, 00:06

Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anawasili leo mkoani Singida, kwa ajili ya kufanya ziara maalumu ya siku mbili. Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone kwa vyombo vya habari ilisema kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni kuhudhuria ibada maalumu ya kumweka wakfu Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya kati, Dk. Alex Seif Mkumbo.

Sherehe hiyo itafanyika makao makuu ya KKKT-Dayosisi ya kati, katika Usharika wa Imanuel mjini Singida, kesho asubuhi.

Dk. Kone alisema, baada ya kushiriki ibada hiyo, Rais ataondoka kuelekea mkoani Tabora, kuendelea na majukumu mengine.

Dk. Kone ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Singida kujitokeza kwa wingi kwenye maeneo yote atakayopita. Mwishoni mwa mwaka jana (Novemba), Rais Kikwete alifanya ziara siku mbili mkoani hapa, ambapo aliweka jiwe la msingi katika mradi wa maji uliopo kijiji cha Mwankoko manispaa ya Singida wa thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 31.5.

Katika ziara hiyo Rais pia alizindua ujenzi wa barabara ya Manyoni-Itigi hadi Chaya (Tabora) Km 89.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami nakampuni ya CHICO ya nchini China kwa gharama ya zaidi ya Sh. bilioni 109.64.

Baadaye akamaliza ziara yake kwa Manyoni mjini kwa kuzindua barabara ya lami Isuna- Manyoni Kl 54 iliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh. bilioni 32.
CHANZO: NIPASHE

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment