Tuesday 22 January 2013

VIJIMAMBO: Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel Nderumaki aogea na viongozi wa PPF

VIJIMAMBO
thumbnail Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel Nderumaki aogea na viongozi wa PPF
Jan 22nd 2013, 22:11

Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Gabriel Nderumaki akiogea na viongozi wa PPF Pensheni Fund wakati walipotembelea TSN kufahamiana na kujifunza mambo mbalimbali katika makutano ya barabara za Nelson Mandela na Nyerere Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw.Steven Alfred,Meneja wa Kanda, Mbaruku Magawa na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
Msanifu kurasa wa gazeti la HabariLeo, Ephraim Mwaluvinga (kulia) akiwaonesha jinsi maadalizi ya gazeti yanavyofanywa kwa ugeni kutoka PPF ulipotembelea chumba habari cha gazeti hilo Dar es Salaam jana.
Mhariri wa Magazeti ya wikiendi ya DailyNews, Ichikaeli Maro akiukaribisha uongozi wa PPF ulipotembelea chumba cha habari cha magazeti hayo. Katikati ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki.
Fundi Mitambo wa TSN, Rashid Singandole, akieleza jinsi mitambo ya uchapaji ya Standard Printers inayomilikiwa na TSN inavyofanya kazi, kwa uongozi wa PPF uliotembelea kiwanda hicho. Kuanzia kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji,Steven Alfred, na Meneja Uhusiano wa Mfuko huo,Bi. Lulu Mengele.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Gabriel Nderumaki (kulia) akiueleza jambo ugeni wa PPF baada ya kutembelea mitambo ya kampuni hiyo muda mchache kabla ya kuondoka.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment