Tuesday 1 January 2013

VIJIMAMBO: Mh. Lowassa azindua VIKOBA kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli

VIJIMAMBO
thumbnail Mh. Lowassa azindua VIKOBA kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli
Jan 1st 2013, 21:10

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli tayari kwa hafla fupi ya uzinduzi wa vikoba katika kijiji hicho.Katikati ni Mkewe Mama Regina Lowassa aliefatana nae kwenye hafla hiyo ya Uzinduzi wa Vikoba.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli walipowasili tayari kwa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba katika kijiji hicho.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake kwa wananchi wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli wakati wa hafla ya uzinduzi wa VIKOBA kijijini hapo.Mh. Lowassa katika hotuba yake,amesema kuwa ushirika wa VIKOBA ni sawa na mshipa wa damu kwa sera ya maisha bora kwa kila Mtanzania,pia alisema kuwa kutokana na kutambua hivyo ushirika wa Vikoba utaanzishwa katika wilaya nzima ya Monduli.Miasha bora kwa kila Mtanzania ni sera aliyoingia nayo madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli,Bi Judith (kulia) akikabidhi kwa Mhe. Edward Lowassa hati maalumu ya uzinduzi wa Vikoba ili ikabidhiwe kwa Wananchi Mswakini Monduli.
Baadhi ya wanachama wa Vikoba wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment