Wednesday 9 January 2013

VIJIMAMBO: MWANAMUZIKI OMAR OMAR AZIKWA KATIKA MAZINGIRA YA VURUGU

VIJIMAMBO
thumbnail MWANAMUZIKI OMAR OMAR AZIKWA KATIKA MAZINGIRA YA VURUGU
Jan 9th 2013, 22:05

Mwili wa marehemu ukisaliwa nyumbani kabla ya kupelekwa makaburini.
'Baadhi ya wasanii wakibadilishana mawazo kabla ya mazishi.
Dully Syaks (katikati) akiwa na mapacha Sunche na Kapeto.
Waombolezaji akina mama.
Baadhi ya wanamuziki wa kizazi kipya.
Mlevi nmmoja akicheza mbele ya waombolezaji.
kwa picha zaidi bofya read more
Umati ukiwa tayari kwenda makaburini.
Wabeba jeneza wakiwa wanatembea kwa magoti.
Vijana waliosababisha vurugu wakisukumana.
Vurugu zikiendelea wakati wa kwenda kuzika.

MWANAMUZIKI mkongwe wa miondoko ya mnanda, Omar Omar Mfungilo, ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana ( Jumatatu) nyumbani kwao Temeke-Mkoroshini amezikwa leo katika makaburi ya karibu na nyumbani kwao.
Mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na watu wengi, yalitawaliwa na vurugu ambazo zilisababisha baadhi ya waombolezaji kuporwa vitu vyao kama simu, pesa, saa na vitu vingine.
Wakati wa kwenda kumzika, vijana waliojiita 'kikosi kazi cha mazishi' waling'ang'ania jeneza lililobeba mwili wa marehemu na kulipeleka wao makaburini huku baadhi yao wakifanya vitendo vya uporaji njiani wakati wa kwenda kumzika.

(PICHA/HABARI NA ISSA MNALLY, GPL)

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment