Thursday 3 January 2013

VIJIMAMBO: MWILI WA SAJUKI WAHAMISHWA MSIKITINI KUTOKA MUHIMBILI

VIJIMAMBO
thumbnail MWILI WA SAJUKI WAHAMISHWA MSIKITINI KUTOKA MUHIMBILI
Jan 3rd 2013, 20:44

MWILI msanii nyota wa filamu, Juma Kilowoko "Sajuki" aliyefariki jana alfajiri, umeondolewa katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya Hospital ya Taifa, Muhimbili.

Na badala yake, mwili wa Sajuki sasa umekwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha msikiti wa Shadhir (Masjid Shadhully) uliopo Kariakoo mtaa wa Sikukuu na Twiga.

Msanii Issa Mussa "Cloud" aliiambia Saluti5 kuwa lengo la kuhamisha mwili huo ni kujaribu kufanikisha taratibu zote za kesho kwenda na muda.

"Muhimbili process za kuchukua mwili ni ndefu na hata
huduma zao za kuosha mwili wa marehemu ni ndefu pia kutokana na wingi wa maiti zinahofadhiwa na kuoshwa hospitalini hapo.

"Hivyo tumeona tuupeleke mwili Masjid Shadhully kwa vile hakuna msongamano kama wa Muhimbili" alisema Cloud. Masjid Shadhully ndio msikiti atakaoswaliwa Sajuki hiyo kesho ambapo mwili wake utachukuliwa msikitini hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa nyumbani kwake Tabata na baadae kurudishwa tena Masjid Shadhully kwa ajili ya kuswaliwa na kwenda kuzikwa makaburi ya Kisutu baada ya swala ya Ijumaa saa 7 za mchana.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment