Monday 14 January 2013

VIJIMAMBO: Q-Chilla "Watu Wasiopenda Maendeleo yangu Ndio Walionifanya Kutumia Madawa ya Lulevya.

VIJIMAMBO
thumbnail Q-Chilla "Watu Wasiopenda Maendeleo yangu Ndio Walionifanya Kutumia Madawa ya Lulevya.
Jan 14th 2013, 20:14


Q Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia.

Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu. Qchilla amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.
Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo.

Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini.

Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia alikuwa aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.

QChilla amesema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani tu na kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo kali.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment