Thursday 17 January 2013

VIJIMAMBO: Serikali yakataa kuunda tume ya kuchunguza Viongozi wa dini kushambuliwa.

VIJIMAMBO
thumbnail Serikali yakataa kuunda tume ya kuchunguza Viongozi wa dini kushambuliwa.
Jan 17th 2013, 21:45

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Suleiman Soraga alipokua amelazwa katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhiombili kufuatia majeraha ya usoni na kifuani yaliyotokana na kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe mjini Unguja juzi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haitounda tume ya kuchunguza matukio ya viongozi wa dini waliojeruhiwa kutokana na kuwa uchunguzi huo unafanywa na jeshi la polisi na bado unaendelea.
Wajumbe hao walitaka serikali kufanya uchunguzi wa matukio mawili yaliotokea hivi karibuni katika matukio ya kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini akiwemo Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga pamoja na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi Padre Ambros Mkenda.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa rais Mohammed Aboud Mohammed aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mwakilishi wa jimbo la Kiwani (CUF)  Hijja Hassan Hijja aliyetaka kuundwa kwa tume ya kuchunguza suala hilo pamoja na kujuwa suala la ulinzi kwa viongozi wa dini na upelelezi wake umefikiya wapi hadi sasa.
Aboud alisema katika hatua zote mbili za uchunguzi wa matukio hayo yanaendelea vizuri sana kazi ambayo inafanywa na taasisi za ulinzi ikiwemo jeshi la Polisi na hakuna sababu ya kuunda tume kwa kuwa uchunguzi huo unafanywa na jeshi la polisi.
"Taasisi za ulinzi ikiwemo Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi wa matukio ya kumwagiwa tindikali sheikh Soraga pamoja na kupigwa risasi kwa padre Mkenda, na sioni kama ipo haja ya kuingilia mamlaka nyengine katika suala hilo, nadhani tuwaachie polisi wafanye kazi hiyo na wakishakamilisha watatupa taarifa kamili ya uchunguzi wao waliofanya"alisema Aboud.
Alisema matukio hayo yameitia wasiwasi mkubwa jamii pamoja na wananchi kwa ujumla kwani yanaonesha wazi kuwepo kwa vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani.
Aboud akitoa salama za mwaka mpya kwa wajumbe na wananchi,aliwataka kuheshimu sheria za nchi na kujiepusha na kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo kuchukuwa sheria mikononi.
Alisema matukio mengi yalijitokeza mwaka jana ikiwemo vurugu za kidini,ambapo inaonesha wazi wananchi kushindwa kuheshimu sheria za nchi.
'Nawaomba wananchi mwaka mpya wa 2013 kuheshimu sheria za nchi na kuacha kujiingiza na vitendo vya vurugu kwa wananchi na kiusababisha uvunjifu wa amani'alisema.
Katibu wa mufti sheikh Fadhil Soraga alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana na kuumiya vibaya sehemu ya so na kulazimika kupelekwa nje ya nchi India kwa matibabu zaidi.
Aidha padre Mkenda alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa anakaribia nyumbani kwake huko Tomondo nje ya mji wa Unguja na kulazimika kusafirishwa hadi Tanzania Bara kwa matibabu zaidi.


You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment