Sunday, 6 January 2013

VIJIMAMBO: YANGA YAENDELEA NA MAZOEZI NCHINI UTURUKI

VIJIMAMBO
YANGA YAENDELEA NA MAZOEZI NCHINI UTURUKI
Jan 6th 2013, 18:50

Nahodha wa Young Africans Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto akisalimiana na wamuzi wa mchezo na nahodha wa timu ya Arminie Bielefeld kabla ya mchezo huo jana.Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence football.
(Picha zote na youngafricans.co.tz)

Kikosi cha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence baada ya jana kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Arminia Bielefeld ambao uliishia kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Adora football Belek - Antalya.
Kocha Brandts ameendelea kukifua kikosi chake na kufanyia marekebisho ya baadhi ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana ambao hata hivyo Yanga iliutawala kwa kipindi chote cha mchezo.
Arminia Bielefeld ambao awali hawakutegemea Tanzania kuwa kunaweza kuwa na timu ambayo inaweza kuwapa upinzania, walikiri mwishoni mwa mchezo kwamba Yanga ina timu nzuri na hawak.utegemea kuona kiwango kizuri cha mchezo kilichoonyeshwa na vijana na wa Jangwnai alisema mmoja wa maofisa wa Arminia Bielefeld.
Ukizingatia Armini Bielefeld ilikuwa imetoka kuifunga Bayern Levekursen 4-2 katika mchezo wa kombe la Ujerumani, walikutana na vijana wa Jangwani ambao waliweza kuutawala mchezo huo kuanzia kwa mlinda mlango Ally Mustafa 'barthez, mpaka kwa washambuliaji wake.
Brandts alisema amefarijika na matokeo ya mchezo huo, japokuwa lengo lake kubwa lilikuwa ni kupata ushindi katika mchezo huo lakini wachezaji wake waliweza kufanya kazi nzuri sana uwanjani kitu kilichofanya Wajerumani kushangaa.
Young Africans mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi, jioni itakua ikifanya mazoezi ya kujenga mwili misuli (GYM) katika Hotel ya Fame Residence Lara & Spa ambao kesho asubuhi itaendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence Football.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment