Saturday, 9 February 2013

VIJIMAMBO: Aliyepanga shambulizi katika bunge la India Afzal Guru anyongwa

VIJIMAMBO
thumbnail Aliyepanga shambulizi katika bunge la India Afzal Guru anyongwa
Feb 10th 2013, 00:37

Muuza matunda mmoja nchini India aliyekuwa amehukumiwa adhabu ya kifo tangu mwaka 2001 kwa kosa la kupanga kufanya shambulizi katika bunge la nchi hiyo amenyongwa. Maafisa wamesema Mohammed Afzal Guru aliyekuwa akisubiri adhabu hiyo tangu 2002 amenyongwa katika gereza la Tihar karibu na Delhi. 
Afzal Guru amekuwa akikana kuhusika na shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu tisa. India imeimarisha ulinzi na kutangaza amri ya kutotembea hovyo katika Jimbo la Kashmir ambako taarifa za kunyongwa huko zingeweza kuzua vurugu. India ni nadra sana kutekeleza adhabu za kunyongwa ambapo Afzal Guru anakuwa mtu wa pili tangu mwaka 2004, baada ya Mohammed Ajmal Kasab.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment