Friday 12 April 2013

VIJIMAMBO: Kukabiliana na tabia nchi

VIJIMAMBO
Kukabiliana na tabia nchi
Apr 13th 2013, 01:00

Salma Said, Mwananchi

ZANZIBAR: Katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, Zanzibar imeanzisha mradi wa kusafisha maji ya chumvi kuwa maji safi na salama kwa wananchi wa vijiji vya Nugnwi Mkoa wa kaskazini Unguja.

Mradi wa huo wa Millioni 500m/= unagharimiwa na serikali ya Japan kupitia mradi wa kukabiliana na athari za tabia nchi- African Adaptation Programme (AAP) chini ya usimamizi wa UNDP

Waziri wa Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar anayeshughulikia (Mazingira) Fatma Abdulhabib Fereji aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana kwamba Zanzibar inakabiliwa na athari za tabia nchi katika maneo mengi ambapo maji safi na yamechafuliwa na maji ya chumvi.


"Wizara yangu imekuwa ikichukuwa hatua mbali mbali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kukabiliana na athari hizo. Zanzibar pia imepata fedha kutoka kwa mfuko maalum wa kusaidia nchi zinazoendlea (LDCF), ambapo fedha hizo zitaelekezwa katik maeneo ya Tumbe, Bwawani, na KIsiwapanza,' alisema fatma.

Waziri Fatma amesema ofisi yake pia, kwa kiasi kikubwa inashirikiana na tasisi nyengine zikiwemo Wizara ya Kilimo na Maliasili, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Asasi za Kiraiya katika kutoa elimu kwa lengo la kupamabana na uharibvifu wa matumbawe ukataji wa miti ovyo na uchimbaji wa mchanga usiofuata taratibu zilizowekwa. .


Akijibu suali la msingi lililoulizwa na mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe CUF katika ukumbi wa baraza la wawakiklishi huko Chukwani nje kidogo na Mji wa Zanzibar .

Aliyehoji Zanzibar ni nchi ambayo kila uchao ardhi yake huwa inapungua kutokana na kuongezeka kwa maji ya Bahari vile vile rutuba yake inakuwa inapungua kutokana na ukataji wa miti ovyo pamoja na utiaji wa mashamba moto katika siku za kilimo .

Kutokana na kuwa kila mwaka idadi ya watu inazidi kuongezeka jambo ambalo husababisha hata zile sehemu zenye rutuba kutumika kwa ajili ya ujenzi ni kwa namna gani wizara hiyo imejipanga katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira na wananchi hasa wakulima waweze kutumia ardhi ipasavyo.

Waziri Fatma alisema katika kukabilian na athari za mabadilijko ya tabia ya nchi ikiwemo kuingia maji ya chumvi kwenye mashamba ya wakulima ofisi ya makamo wa kwanza imekuwa ikwaelimisha na kuwashajihisha wadau na wananchi wa maeneo yaliyoathiriwa kupanda miti kwa wingi na ikibidi kujenga matuta ili kupunguza athari hizo na kupata nafasi ya kuendeleza kuyatumia maeneo hayo kwa shughuli za kilimo.

Maeneo ambayo tayari yamejengwa matuta kwa ajili ya kuzuiya maji ya chumvi ni pamoja na Koowe,Ukele,Tumbe na kwa Jimbwa ilioko Kengeja .

"Hivi karibuni ofisi ya makamo wa kwanza wa rais imeshirikiana na jumuiya ya uhifadhi na maendeleo ya jamii (CODECOZ) katika kutayarisha vitini vya muongozo wa sera sheria na kanuni za mazingira kwa wana jamii na aasasi za kiraiya"alisem Waziri huyo.

Kwa sasa muongozo huo umeshafundishwa kwa wakufunzi 75 kutoka wilaya ya Mkoani ,micheweni Kaskazini A na B, ambapo mafanikio yamekuwa ni makubwa mno kwani jamii imekuwa na mwamko mkubwa wa kimazingira ambapo jumuiya za kiraiya kamati na vikundi vingi vya jamii kulinda na kuhifadhi mazingira vimeanzishwa Unguja na Pemba.

Juhudi za utoaji wa elimu zimepelekea kuanzishwa kwa mtandao wa mazingira Zanzibar am bao unaundwa na jumuiya kumi na moja za mazingira ziliopo maeneo mbali mbali ya Zanzibar ,mafanikio hayo pia yamepelekea kuundwa kamati za mazingira za uvuvi katika sehemu nyingi za Unguja na Pemba na kushirikiana na serikali katikia doria za baharini ili kupambana na uvuvi haramu.



You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment