Sunday 21 April 2013

VIJIMAMBO: Movie Star wa Nollywod Tonto Dikeh akanusha taarifa za kwenda BBA.

VIJIMAMBO
Movie Star wa Nollywod Tonto Dikeh akanusha taarifa za kwenda BBA.
Apr 22nd 2013, 01:33


Movie star mwenye vituko kutoka Naija Tontoh Dikeh ameziruka futi kumi na mbili stori zinazomhusisha na kuiwakilisha Naija kwenye lile shindano maarufu barani Afrika la Big Brother .
Tonto Dikeh alivumishwa kuwa mshiriki atakayeiwakilisha Naija kwenye Big Brother ya mwaka huu jambo ambalo liliwafurahisha mafans wa shindano hilo ambao walikuwa na hamu ya kuona vitu atakavyofanya staa huyo ambaye ana vituko vingi kwenye maisha yake ya kawaida .
Tonto akitumia akaunti yake ya mtandao wa twitter alikanusha story hizo akisena kuwa ni za uongo na hafahamu zilikoanzia . Tweet ya staa huyo ilinukuliwa ikiwa na maneno haya "Lol how ya'll tink i'm gonno go in2 Bb8 Houze? Sure beats mii. Kip d rumour alive but know in ur hearts dat na lie ."
Star huyo aliongeza kuwa walioanzisha uvumi huo ni waandishi wa habari za udaku kwenye mitandao yaani Gossip Bloggers ambao siku zote hutafuta jinsi ya kuwavutia wasomaji hadi kudiriki kutunga stori za uongo.
Taarifa hizo zilithibitishwa na afisa uhusiano wa Mnet na Africa Magic Nigeria Yinka Epega ambaye alisena kuwa taarifa zozote abazo hazijathibitishwa na kampuni ya Mnet kupitia kwa wasemaji wake rasmi zisitiliwe maanani kwani si za ukweli.
Tonto Dikehh ambaye hivi karibuni aliingia rasmi kwenye upande mwingine wa masuala ya burudani yaani muziki amekuwa akiandikwa sana na vyombo vya habari nchini Naija kutokana na vituko vyake na watazamaji wa BBA walijawa na shauku kubwa ya kumuona nyota huyu atafanya nini akiingia kwenye jumba la BBA na taarifa hizi za kukanushakwake zitakuwa zimewasononesha wengi.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment