Account ya mtandao wa kijamii ya Twitter ya mwanamuziki maarufu Afrika kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya (AY) yatambulika rasmi na kuwa mwanamuziki wa kwanza hapa Bongo account yake kutambulika yaani (Verified Account) .
Twitter ambayo hufanya hivyo kwa kukuwekea alama ya tick ya blue mbele ya jina lako ili kukutambulisha kwa marafiki, ndugu, jamaa, mashabiki wako wanaokufuata [followers] kuwa wewe ni mtumiaji halisi wa account hiyo walifanya hivyo kwenye account ya Ambwene ndani ya masaa kadhaa yaliyopita.
Twitter pia hufanya hivi ili kukutofautisha na watumiaji wengine wanaoweza kutumia jina lako katika mtandao huo na wamekuwa wakifanya hivyo kwa watu maarufu katika nyanja mbalimbali.
AY amekuwa mmoja kati ya watanzania wachache ambao account zao zimekuwa hivyo akiwemo mcheza kikapu wa Oklahoma City Thunder(OKC) Hasheem Thabeet [@hasheemthedream], Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete [@jmkikwete] Flaviana Matata [@FlavianaMatata] na Waziri January Makamba
No comments:
Post a Comment