Friday 5 April 2013

VIJIMAMBO: WIZARA YA AFYA ANGALIENI WIZI HUU WA VYANDARUA

VIJIMAMBO
thumbnail WIZARA YA AFYA ANGALIENI WIZI HUU WA VYANDARUA
Apr 5th 2013, 23:29



Katika hali ambayo si yakufumbuwa macho na Serikali kupitia Wizara ya Afya ni juu ya uuzwaji wa vyandarua (NET) za kujikinga na Mbu waambukizao ugonjwa wa Malaria ambazo ni za msaada.



 Maneno ya NOT FOR SALE yakiwa yamekatwa katwa ili kuwababaisha wananchi kuwa si za kugaiwa bure.
Mfuko wa kuhifadhia Net hiyo ya msaada.

Vyandarua hivyo vya Olyset Net ambazo ni maalum kwaajili ya kugaiwa bure kwa watu waliokatika uhitaji hasa wakina mama wajawazito sasa vinauzwa mitaani na serikali inatakiwa kufanya msako wa kubaini wafanya biashara wanaouza vyandarua hivyo kinyume cha sheria.

Olyset Net ni vyandarua vya msaada kutoka UKaid, Wizara ya Afya ya Kenya na Shirika la PSI Kenya na katika mifuko yake imeandikwa FREE NET na maneno mengine ya NOT FOR SALE na UUZWAJI HAURUHUSIWI.

Lakini ili kuhalalisha uuzwaji huo wauzaji hao ambao wanaibia wananchi wameamua kukata maeneo yote yaliyo na maneno hayo na pindi mteja akifika huuziwa kwa Tsh 6,500/= bila punguzo la aina yeyote.

Maeneo zinapouzwa sana Vyandarua hivyo ni katika magari madogo yanayosimama katika vituo daladala na mikusanyiko mikubwa ya watu nyakati za jioni.

Uchunguzi wa Father Kidevu Blog umethibitisha kuwapo kwa biashara hiyo katika maeneo ya Ubungo, Buguruni, Gongo la Mboto na maeneo mengine kama Mbagala na Mwenge jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi wameitaka Serikali kuwakamata mara moja wauzaji hao wa vyandarua hivyo vinavyopaswa kugaiwa katika maduka ya HATI PUNGUZO lakini kutokana na biashara hiyo vimekuwa havipatikani katika maduka hayo.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment