Tuesday 5 February 2013

VIJIMAMBO: OMAN YAISAIDIA ZANZIBAR

VIJIMAMBO
thumbnail OMAN YAISAIDIA ZANZIBAR
Feb 5th 2013, 23:17

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akisalimiana na Dk.Rawya Saud Al Busaid,Waziri wa Elimu ya Juu wa Nchini Oman,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Waziri wa Elimu ya Juu wa Nchini Oman,Dk.Rawya Saud Al Busaid,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu,Sayansi na
 Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas,akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanziba
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
 Irina Bokovas,akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
 Irina Bokovas,pamoja na ujumbe aliofuatana nao walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo. 

Picha zote kwa hisani ya SALMA SAID
Na Salma Said, ZANZIBAR

SERIKALI ya Oman imeeleza azma yake ya kuendelea kuinga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kuanzia na elimu ya juu kupitia Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).
 
Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Dk. Rawya Saud Al Busaid, aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu Mjini Zanzibar.
 
Katika maelezo hayo, Waziri Dk. Rawya alimueleza Dk. Shein kuwa akiwa Zanzibar yeye na Ujumbe wake utapata nafasi ya kujadili zaidi Makubaliano ya Awali  ya mashirikiano kati ya Zanzibar na Oman kupitia sekta ya elimu yaliotiwa saini katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ziara yake nchini humo hivi karibuni.
 
Dk. Rawya alieleza kuwa Serikali ya Oman imetoa ahadi ya kuwapatia nafasi wanafunzi wa Zanzibar katika Nyanja mbali mbali za masomo kupitia Mfuko wa Mfuko wa Maendeleo ya Elimu wa Sultan Qaboos kwa ajili ya Zanzibar  (SQAP).
 
Alisema kuwa katika mchakato huo Chuo Kikuu hicho cha Taifa cha Zanzibar ndio kitakachoamua ni eneo gani kitataka kuimarishwa zaidi kwani tayari Serikali hiyo ya Oman imeshajipanga vyema kutoa ushirikiano huo kwa chuo hicho ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi za masomo ya Uzamili na Uzamifu.
 
Dk. Rawya alisema kuwa katika Mpango wa Muda mrefu Serikali hiyo ya Oman itajikita zaidi katika kuunga mkono kwenye maeneo makuu matatu ikiwa ni pamoja na kukisaidia Chuo hicho cha SUZA.
 
Pia, kusaidia taasisi mbali mbali za serikali ambazo baadae zitakuwa ni sehemu ya chuo kikuu hicho na kuasaidia wanafunzi watakaomaliza masomo ya Sekondari kuwapa nafasi za masomo katika vyuo mbali mbali duniani ili baadae waje kutoa utaalamu wao katika Chuo Kikuu hicho.
 
 
Aidha, Waziri huyo wa Elimu wa Oman alisema kuwa Oman pia, ina mpango wa kuiunga mkono Serikali katika kuwapatia wanafunzi wa Zanzibar nafasi za masomo katika vyuo vikuu mbali mbali duniani gharama ambazo zote zitatolewa na nchi hiyo na kupata huduma zote zinazostahiki za kimasomo kama anazozipata mwanafunzi wa Oman.
 
Dk. Rawya alisema kuwa mipango ya Serikali ya Oman katika kukiimarisha chuo hicho Kikuu cha SUZA ikifanikiwa chuo hicho kinaweza kupatanafasi maalum ndani ya serikali hiyo ya Oman ambapo chuo hicho kitaweza kuunganishwa na vyuo kadhaa duniani na kuweza kupata mafanikio.
 
Sambamba na hayo, Dk. Rawya alimueleza Dk. Shein kuwa  kuna wananchi wengi wa Oman wenye asili ya Zanzibar ambao wako tayari kuiunga mkono Zanzibar na kutoa misaada yao mbali mbali lakini bado hawajajua taratibu zilizopo ili kufanikisha azma yao hiyo kwa ndugu zao wa Zanzibar.
 
Alieleza kuwa Waomani waliowengi ambao wanaasili ya Zanzibar wamevutiwa kuisaidia Zanzibar katika sekta ya afya ikizingatiwa kuwa kuna Madaktari wengi nchini humo wenye asili ya Zanzibar wakiwemo Madaktari Bigwa.
 
Nae Dk. Shein kwa upande wake alieleza kuwa Zanzibar inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati yake na Oman huku akisisitiza kuwa azma ya nchi hiyo kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya elimu kupitia SUZA ni jambo la busara na lenye matumaini makubwa katika maendeleo ya Zanzibar
 
Dk. Shein pia, alieleza kuvutiwa kwake na hatua ya nchi hiyo ya kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya afya na kusisitiza kuwa kupitia Idara maalum ya Diaspora aliyoinda katika afisi yake kutaandaliwa utaratibu maalum wa jinsi ya kuwasiliana na wataalamu hao na baadae wizara ya Afya itafanya taratibu husika.
 
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alitoa ahsante kwa ujio wa Waziri huyo hapa Zanzibar huku akisisitiza uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya pande mbili hizo utaimarishwa.
 
Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Ali Juma Shamuhuna alisema kuwa Waziri huyo wa Elimu akiwa na Ujumbe wake huo upo nchini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano mwema na Zanzibar katika sekta ya elimu.
 
Alisema kuwa ujumbe huo tayari umeshafanya ziara ya kukitembelea Chuo hicho cha SUZA pamoja na kuwa na azma ya kutembelea taasisi nyengine za elimu zikiwemo Chuo cha Afya, Skuli ya Lumbumba na nyenginezo huku baadhi ya wajumbe wakiahidi kwenda kisiwani Pemba ili kuangalia maendeleo katika sekta hiyo ya elimu nchini.
 
Wakati huo huo, Dk. Shein alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Mama Irina Bokova, ambapo Shirika hilo limeeleza azma yake ya kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo elimu, Uhifadhi wa Mji Mkongwe Kimataifa, Utamaduni, Mazingira na mengineyo.
 
Nae Dk. Shein kwa upande wake alitoa pongezi kwa Mama Bokova kwa ujio wake hapa nchini na kutoa pongezi kwa Shirika hilo kutokana na juhudi zake za kuiunga mkono Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo.
 
Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Mkurugenzi Mkuu huyo kuwa   Zanzibar imevutiwa na juhudi za UNESCO katika uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar na kusisitiza haja ya kuyafayia ukarabati majnego ya mji huo ikizingatiwa kuwa ni kivutio kikuu cha watalii wanaoitembelea Zanzibar.


You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment