Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde, Mohammed Dewji amesema iwapo Taifa Stars itafuzu kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, zawadi yao itakuwa gumzo.
Dewji maarufu kama Mo alisema zawadi ya Stars tayari imeandaliwa lakini inabaki kuwa siri katika kipindi ambacho vijana wanapambana.
"Lakini tumetoa shilingi milioni thelathini kama hamasa na zawadi kwa kufikia hapa walipo.
"Tunaamini wanaweza kuvuka hapa walipo wakipambana zaidi. Tunawashauri waendelee kuwa na nidhamu, malengo na waamini kwamba wana jukumu kubwa kuwawakilisha Watanzania," alisema Dewji.
Dewji amesema ataongozana na wadau kadhaa akiwemo Zitto Kabwe kwenda Marrakesh, Morocco kuungana na kikosi cha Stars ambacho kitakuwa kinapambana nchini humo kuhakikisha kinashinda.
Morocco lazima watakuwa wamejiandaa kutokana na hasira za kuchapwa mabao 3-1 na Stars katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, hivi karibuni. Maelezo kwa hisani ya Saleh Ally
No comments:
Post a Comment