Monday, 20 May 2013

VIJIMAMBO: Mjadala wa waTanzania UK Kufanyika University of Reading!

VIJIMAMBO
thumbnail Mjadala wa waTanzania UK Kufanyika University of Reading!
May 21st 2013, 00:01

Siku ya Jumamosi tarehe 01/06/2013, waTanzania waishio UK watakutana kwa ajili ya mjadala mkubwa utakaohusu mwaswala yafuatayo: Elimu; Katiba;Muungano; na Utaifa. Mjadala utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa University of Reading. Hii ni nafasi ya kipekee kwa waTanzania kuzungumzia mambo muhimu yanayoihusu jamii yetu bila kujali itikadi, imani, rangi au kitu kingine chochote. Vikundi mbali mbali vya kidini, kisiasa na kijamii vitakuwepo.

Japokuwa mjadala unafanyikia UK, waTanzania wote wenye nia ya kushiriki kutoka mahali popote pale duniani wanaweza na wanakaribishwa kushiriki. Kama ungependa kushiriki kutoka sehemu yoyote ulipo, unaweza kufanya hivyo kwa kupitia tweeter account itakayotolewa hivi karibuni.

Mjadala utarushwa kwenye YouTube channel. Pia kwa hisani ya Funguka Forums mjadala utakuwa unarushwa live kwenye fungukaforums.com. Pia updates zitakuwa zikitolewa kwa kupitia facebook na twitter.

Karibuni wote tushiriki kwa mapenzi ya nchi yetu.

"Usiulize Tanzania imekufanyia nini. Jiulize wewe umeifanyia nini nchi yako. "


You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment