Monday 7 January 2013

VIJIMAMBO: Irene Uwoya na Jackline Wolper Ndani ya Beef Tena-Chanzo Hichi Hapa

VIJIMAMBO
thumbnail Irene Uwoya na Jackline Wolper Ndani ya Beef Tena-Chanzo Hichi Hapa
Jan 7th 2013, 17:40



'BODIGADI' wa mwigizaji kiwango Bongo, Irene Uwoya, aliyetajwa kwa jina moja la Mariam anadaiwa kumshushia kipigo mwigizaji Jacqueline Wolper chanzo kikidaiwa kuwa ni mwendelezo wa bifu lililokuwa limefifia kati ya mafahari hao wa sinema za Kibongo.


Kwa mujibu wa chanzo makini, sheshe hilo lilitokea Desemba 31, mwaka huu (mkesha wa mwaka mpya) katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar, wakati mastaa mbalimbali walipokuwa wakisherehekea kuupokea Mwaka Mpya wa 2013.
MUVI LILIVYOANZA
Chanzo hicho makini kiliweka 'pleini' kuwa, wakati shamrashamra za mwaka mpya zikiendelea, ghafla bodigadi huyo wa Uwoya, alimvaa Wolper aliyekuwa anacheza muziki na kuanza kumvuta cheni yake kisha kumshushia kipigo 'hevi'.
"Mariam na Uwoya walikuwa wamekaa pamoja wakipiga kilevi na kustorisha, ghafla tukashangaa mpambe huyo ameinuka na kwenda kumvaa Wolper ambaye alikuwa bize kucheza muziki," kilisema chanzo hicho na kuongeza:
"Uwoya atakuwa kamtuma kwa sababu haiwezekani wakae wote halafu dakika chache mbele, ainuke na kwenda kumfanyia fujo mwenzake (Wolper). Hapa kuna kitu."
UWOYA AMKANA BODIGADI
Tofauti na ilivyodhaniwa na wengi kwamba bodigadi huyo alitumwa na Uwoya, baada tukio hilo Klabu ya Bongo Movie Unit iliitisha kikao cha dharura ambapo ilidaiwa kuwa Uwoya alikana kuhusika na akamlaani Mariam kwa kitendo hicho cha kumfanyia vurugu Wolper.
"Wasani wengi walijua Uwoya ndiye aliyetengeneza mchongo mzima lakini kikao kimekataa na kumuona Mariam ndiye mkosaji," kilisema chanzo hicho.


WOLPER ANASEMAJE?
Baada ya kusikia maelezo ya kikao cha klabu, paparazi wetu alimtafuta Wolper na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alijibu kwa kifupi:
"Siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo, watafuteni viongozi wetu," alisema Wolper.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Kumbukumbu inaonesha mwaka jana, mastaa hao waliwahi kuwa ndani ya bifu zito ambapo baadaye walipatanishwa na mdau wa burudani maarufu kwa jina la Daudi Kipunguni maeneo ya Mlimani City jijini Dar.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment