Thursday 3 January 2013

VIJIMAMBO: YANGA KUIVAA ARMINIA BIELEFELD JUMAMOSI

VIJIMAMBO
YANGA KUIVAA ARMINIA BIELEFELD JUMAMOSI
Jan 3rd 2013, 23:25

Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini katika viwanja vya Fame Residence leo asubuhi
Timu ya Young Africans Sports Club yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam nchini Tanzania siku ya jumamosi itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya kutoka nchini Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya.
Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani ambayo pia imekuja kambi ya mafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la pili nchini Ujerumani.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo inawachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
Unajua tuna siku tano (5) tangu tufike hapa mjini Antalya Uturuki na tumeshafanya mazoezi kwa siku nne (4) hivyo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu alisema 'Brandts'
Haruna Niyonzima & Athumani Idd 'Chuji' wakiwa mazoezini leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence Football
Arminia Bielefeld imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na timu ya Young Africans ambao ni mabingwa mara 23 katika ligi kuu ya Tanzania.
Leo asubuhi Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa siku ya jumamosi mjini Antalya.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.

Aidha kuhusu hali ya hewa leo jua linawaka toka asubuhi mpaka hivi sasa na kwa leo ni sentigred 23 mpaka 25, hivyo hali ya hewa ni nzuri kabis ana jua linawaka.
Wachezaji wakiendelea na mazoezi leo asubuhi

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment