Tuesday 2 April 2013

VIJIMAMBO: BYC II YAWASILI NCHINI TAYARI KUWAKABILI AZAM FC J'MOSI, WACOMORO KUCHEZESHA MECHI

VIJIMAMBO
BYC II YAWASILI NCHINI TAYARI KUWAKABILI AZAM FC J'MOSI, WACOMORO KUCHEZESHA MECHI
Apr 3rd 2013, 00:17

Kikosi cha BYC II kikiwasili jijini Dar es Salaam.

BYC II Imewasili leo jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wake wa CAF Confederations Cup dhidi ya Azam FC utakaochezwa Jumamosi tarehe 6/04/2013. Viingilio Mzunguko itakuwa Tsh 2,000, wakati VIP A itakuwa 20,000, VIP B&C itakuwa 10,000 na Orange itakuwa 5,000.
Kikosi cha Azam FC.

Release No. 056
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 2, 2013

Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi watakaochezesha mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na Barrack Young Controllers II ya Liberia itakayochezwa Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi wa kati ni Adelaide Ali, mwamuzi msaidizi namba moja ni Amaldine Soulaimane wakati Ibrahim Mohame atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ansudane Soulaimane.
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni atakuwa Abdelhamid Radwan kutoka Misri. Maofisa hao wa mechi hiyo watafikia kwenye hoteli ya Holiday Inn.
Wakati huo huo, Barrack Young Controllers II imewasili nchini leo (Aprili 2 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Nairobi, Kenya inapounganisha safari hiyo inayoanzia Monrovia kupitia Accra, Ghana.
Timu hiyo iliyofia hoteli ya Sapphire Court itafanya mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake kwa ajili ya mechi hiyo huku wapinzani wao Azam wakiendelea kujinoa kwenye uwanja wao wa Azam Complex.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment