Tuesday 2 April 2013

VIJIMAMBO: Waziri Mkuu Pinda Ahudhuria Misa ya Pamoja Jijini Arusha Kuaga Marehemu Waliofikwa na Mauti Baada ya Kufukiwa na Kifusi Jana

VIJIMAMBO
thumbnail Waziri Mkuu Pinda Ahudhuria Misa ya Pamoja Jijini Arusha Kuaga Marehemu Waliofikwa na Mauti Baada ya Kufukiwa na Kifusi Jana
Apr 3rd 2013, 00:54


Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha. Maporomoko hayo yametokea jana na kusababisha vifo vya watu13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru
Waziri Mkuu akiwa na wabunge wa Arusha na Meya pamoja na mkuu wa mkoa kwenye msiba huo mzito. Toka Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulongo, Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari na Mbunge wa kuteuliwa Catherine Magige
Sehemu ya majeneza ya marehemu katika ibada hiyo maalumu leo
Waziri mkuu Mizengo pindaakiongea na familia, ndugu na jamaa wa marehemu walioporomokewa na moramu.
Kiongozi wa dini akiombea marehemu waliofariki kwa kuporomokewa na Moramu

Waziri Mkuu akipeana mkono na Askari wa Jeshi la Wananchi (jwtz) alipotembelea eneo la tukio. 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasili mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Maunti meru.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoka eneo la tukio katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili.

Picha zote na Chris Mfinanga

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment