Monday, 4 February 2013

VIJIMAMBO: MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AANZA RASMI ZIARA YAKE KWA KUKUTANA NA MAWAZIRI JIJINI DAR LEO

VIJIMAMBO
MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AANZA RASMI ZIARA YAKE KWA KUKUTANA NA MAWAZIRI JIJINI DAR LEO
Feb 4th 2013, 23:06

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Bi. Irina Bokova's (kushoto) akitoka katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro akiwa ameambatana na Msaidizi wake pamoja Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka (kulia) tayari kuanza rasmi ziara yake nchini mapema leo asubuhi.
Bi. Irina Bokova's akiingia kwenye gari tayari kuanza rasmi ziara yake.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka kabla ya kuanza mkutano na Menejimenti ya Umoja wa Mataifa nchini katika Ofisi za Shirika la UNESCO Tanzania. Kushoto ni Bi. Irina Bokova's.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (kushoto) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's ( wa pili kushoto) ofisini kwa Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (kulia) kabla ya kuanza mkutano na Menejimenti ya Umoja wa Mataifa pamoja na wafanyakazi wa Ofisi za UNESCO Tanzania.
Dkt. Alberic Kacou akizungumza jambo na Bi Irina Bokova's kwenye ofisi za UNESCO Tanzania mapema leo asubuhi.
kwa picha zaidi bofya read more

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.Irina Bokova's akisalimiana na baadhi ya viongozi wa matawi ya Umoja wa Mataifa nchini kabla ya kuanza kwa mkutano.
Bi. Irina Bokova's akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa matawi ya Umoja wa Mataifa nchini.
Bi.Irina Bokova's akiendesha kikao cha Menejimenti ya Umoja wa Mataifa nchini na kugusia Agenda muhimu za kuboresha sekta ya Elimu nchini. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen.
Mkutano ukiendelea.
Baadhi ya viongozi wa matawi ya Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.Irina Bokova's na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka wakiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Menejimenti ya Umoja wa Mataifa nchini.
Bi. Irina Bokova's akisalimiana na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin wakati wa mkutano na wafanyakazi wa UNESCO uliofanyika katika Ofisi za shirika hilo nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akimsalia mmoja wa wafanyakazi wa UNESCO Tanzania Bi. Rahma.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi za UNESCO nchini wakisikiliza nasaha za Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's (hayupo) mapema leo asubuhi.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj (kushoto) akimuongoza kuelekea kwenye chumba cha mikutano kuzungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaa.
Bi. Irina Bokova's akisalimiana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa.
Bi.Irina Bokova's akiwa kwenye mkutano na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa ( wa pili kushoto) na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) wakijadili changamoto mbalimbali na mbinu mbadala za kunyanyua sekta ya elimu nchini kwa kusaidia na Shirika lake la UNESCO.
Bi.Irina Bokova's akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Bi.Irina Bokova's akifanyiwa mahojiano na Capital Television baada ya mkutano wake na mawaziri hao.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova's akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa tayari kuelekea visiwani Zanzibar.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment