Kama anamfahamu msanii wa muziki wa kizazi kipya Mzungu Kichaa katika gemu basi hivi sasa kuna mzungu mwingine anayeitwa Badawi, ambaye ameibuka nchini Tanzania kuwashika mashabiki wa miondoko hiyo ambapo licha ya kufokafoka jamaa anafanya pia miondoko ya reggae.
Badawi Poa mzaliwa wa nchini Ujerumani ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam aliye chini ya label ya Kama Kawa Records, ambaye kwa uzoefu wake wa miezi minane Tanzania, ameamua kuandika ngoma kuhusiana na hali halisi ndani ya daladala Tanzania ambapo wasafiri hulazimika kujaa hadi kusimama na kushikilia bomba ndani ya gari ili kuweza kufika katika mizunguko yao tofauti tofauti.
Msanii huyu ameipatia kazi hii jina 'Shika Bomba' na Jumamosi hii anatarajia kuiachia video yake akiwa na matumaini makubwa ya kufanya poa katika game ya bongo flava Tanzania. Inspiration yake kubwa ikiwa ni wasanii kama vile Professa Jay, Lady Jay Dee na wengineo.
No comments:
Post a Comment