Friday, 3 May 2013

VIJIMAMBO: RAIS KIKWETE AMPOKEA RAIS WA SERIKALI YA MPITO YA MADAGASCAR JIJINI DAR LEO

VIJIMAMBO
thumbnail RAIS KIKWETE AMPOKEA RAIS WA SERIKALI YA MPITO YA MADAGASCAR JIJINI DAR LEO
May 3rd 2013, 23:23

Rais Dkt . Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mhe. Andry Rajoelina aliyewasili jioni ya leo Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini,katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Kikwete, akiongozana na Rais huyo baada ya kumpokea.
Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili mjini Dar Es Salaam jioni ya leo , Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya
kikazi ya siku mbili.


Amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es Salaam na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.


Viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo baadaye leo Ikulu, Dar Es salaam.


Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari mwaka huu.


Rais Kikwete alipokutana mara ya mwisho na Rais huyo wa serikali ya mpito ya Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Rais Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi Rais wa zamani wa Madagascar Mhe Marc Ravalomanana asigombee katika uchaguzi mkuu huo. Picha kwa hisani ya Sufianimafoto

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment