Tuesday 29 January 2013

VIJIMAMBO: MABIGWA WA TETEZI WA AFCOM WAFUNGASHWIA VILAGO UKO KWA MADIBA

VIJIMAMBO
MABIGWA WA TETEZI WA AFCOM WAFUNGASHWIA VILAGO UKO KWA MADIBA
Jan 29th 2013, 22:41

Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika

Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa bingwa barani Afrika, Chipolopolo ya Zambia, leo wamebaunduliwa nje ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika baada ya kutoka sare 0-0 na Burkina Faso katika mechi yao ya mwisho ya makundi.

Burkina Faso imeanza mechi hiyo kwa bahati mbaya baada ya nyota wake Alain Traore kupata jeraha na kuondolewa uwanjani baada ya dakika kumi pekee.
Traore amefunga magoli matatu zikiwemo mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Ethiopia ambayo walishinda kwa magoli manne ya yai.
Dakika chache baadaye Davis Nkausu, wa Zambia vile vile alijeruhiwa na kuondolewa uwanjani na mahala pake kuchukuliwa na Joseph Musonda baadda ya kugongana na mlinda lango wa Burkina Faso.
Kufikia wakati wa mapunziko timu hizo mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ya kutofangana bao lolote.
katika kipindi cha pili Zambia ilifanya mashambulio kadhaa katika lango la Burkina Faso, lakini juhudi zao zligonga mwamba.
Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili zikigawamna alama moja kila moja na hivyo Burkina Faso kusonga mbele baada ya kukusanya jumla ya alama tano nayo zambia ikiridhika la alama mbili.
Nigeria imeongoza kundi hilo kwa jumla ya alama tano huku Ethiopia ikivuta mkia na alama moja.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment