Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali ya Zanzibar imeeleza changamoto kadhaa ambazo zinakabili ofisi nyingi za umma ikiwa pamoja na kutofuatwa kwa sheria za fedha na manunuzi.
Hayo amebainishwa na Ismail Jusa Ladhu katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakati akiwasilisha muhtasari wa ripoti ya kamati ya kudumu ya katiba na sheria kuhusu utendaji katika baadhi ya wizara za serikali kwa mwaka 2012/2013
Alisema serikali imekuwa ikichelewa kuchukuwa hatua juu ya mambo yanayobainika katika ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Seikali mfano, uelewa ndogo wa wadau kuhusu ripoti za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali.
"Ni muhimu wadau, na wananchi kwa jumla wakaelimishwa kuhusu ripoti za mkaguzi na kupewa fursa za kutoa maoni yao kwa lengo la kuleta ufanisi," alisema Jussa ambaye ni makamo mwenyekiti wa kamati hiyo.
Jambo jengine ambalo serikali ni lazima ilifanyie kazi ni kutokuwepo mashirikiano mazuri baina ya afisi hii (ya Mkaguzi) na Wizara ya nchi (AR) utumishi wa umma na utawala bora na kusababisha kupungua kwa ufanisi katika ofisi mbili hizo.
Jussa alisema "Yote hayo yamebainika baada ya kamati ya katiba na sheria na utawala kutembelea katika ofisi hizo, lakini pia kamati inashauri Serikali kuzichukulia hatua za kinidhamu Wizara, Mashirika pamoja na tasisi zisizowasilisha hesabu zao za mwaka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ikiwa na maelezo ya ubabaishaji."
Aidha Jussa kwa niaba ya kamati alisema kamati yake inasisitiza agizo la kutaka mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali kuimaisha utendaji na kufanya ukaguzi yakinifu na wa kina ili kuweka wazi ubadhirifu katika taasisis za serikali bila woga.
Mwakilishi huyo alisema haipendezi kuona serikali inakaa kimya bila kuchukuwa hatua baada ya kamati ya kuchunguza hesabu kugundua matumizi mabaya na vyelelezo ambayo hayaonekani katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali.
No comments:
Post a Comment