Thursday 2 May 2013

VIJIMAMBO: Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited wasaini makubaliano

VIJIMAMBO
thumbnail Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited wasaini makubaliano
May 3rd 2013, 01:23

Leo tarehe 02 Mei 2013, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited wamesaini makubaliano ya awali ya kumiliki kwa pamoja eneo la kitaru C, Mirerani kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya tanzanite. Umilikaji huo utakuwa wa asilimia 50 kwa 50 kati ya pande hizo mbili. Waliosaini makubaliano hayo ni Bw. Gray L. Mwakalukwa ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO na Dr Bernard Olivier, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited.
Makubaliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Uchoraji Ramani za kijiolojia uliopo Wakala wa Jiolojia Tanzania- DODOMA.
Picha na Samwel Mtuwa

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment