Thursday 14 March 2013

VIJIMAMBO: KAMBI MBWANA: SITAISAHAU SIKU YA LEO KATIKA MAISHA YANGU

VIJIMAMBO
thumbnail KAMBI MBWANA: SITAISAHAU SIKU YA LEO KATIKA MAISHA YANGU
Mar 14th 2013, 23:10

Kambi Mbwana akilishwa keki na mmoja ya wafanyakazi wenzake.
Keki ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Kambi Mbwana. Kambi alisema, "Hii ni siku yangu muhimu mno. Zaidi, inanifanya niamini kuwa bado tunapaswa kuishi kwa amani na upendo, ukizingatia kuwa sijatoa hata mia yangu. Huu ni upendo wa aina yake kutoka kwa Mwani Nyangassa na wafanyakazi wote wa New Habari 2006 Ltd,".


KUTOKA KWA KAMBI MBWANA

NIKABAKI kimya. Sikuwa na neno la kusema, zaidi ya kutumbua macho yangu, kama vile natafuta panya aliyechukua pochi yangu yenye mia tano ya kunifikisha kwenye msiba wa ndugu au mtu mwingine wa karibu na mimi.

Ndivyo ninavyoweza kuielezea siku hii, tukio la kushtukizwa la kupewa keki katika kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa, ninayoadhimisha kila Machi 14. Nakumbuka, niliinuka kwenye kiti change, nikitoka nje, ambapo ghafla nikasikia wimbo huu, Happy Birthday Kambi.

Sauti thabiti kutoka kwa akina dada hawa wawili, Mwani Nyangassa, ambaye licha ya kuwa ni dada yangu wa karibu mno, ila kikazi pia ni bosi wangu, akiwa sambamba na mwanadada Jenifer Ullembo, wote tukiwa kwenye Kampuni ya New Habari 2006 Ltd.

Pamoja na kudanganywa kikao na bosi wangu Mwani Ngangassa, lakini pia najiuliza gharama za keki hii imetoka kwa ajili ya Kambi Mbwana. Hakika, natumia muda mwingi kufikiria namna gani ya kuwalipa watu hawa kwa moyo wao wa upendo.

Nashukuru, zaidi nikihakikisha kuwa kuwa katika kipindi cha uhai wangu, kuna mengi ambayo aidha kwa wakati mwingine hayakuwa mazuri, lakini wafanyakazi hawa waliniunga mkono na kunifariji. Hakika haya ni matukio makubwa mno.

Huwatokea watu mara chache mno kwa mwaka, maana tukio la leo ni kati ya yale ambayo nitakabi nayawaza katika kipindi change cha maisha ya duniani. Nakumbuka kauli ya dada Mwani Nyangassa, akiitoa kama bosi, Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Mtanzania.

"Kambi usiende popote tuna kikao leo kujadili utendaji wetu wa kazi," ilikuwa kauli ya kuelezea kuwa kumbe muda ujao tungekaa na kujadili kazi zetu. Sawa, lakini huyu naye aliniambia, anaitwa Mohamed Mharizo kuwa, umeambiwa kuhusu kikao, basi usiende popote Mkurugenzi wa Handeni Kwetu," alisema Mharizo.

Sikujua lolote zaidi ya kusema asante, sitakwenda popote zaidi ya kusubiria kikao hicho baada ya muda wake kufikia. Haya ndio maisha. Haya ndio matokeo ya kuishi kwa upendo na watu wote bila kuangalia ni mtu wa aina gani.

Natumia fursa hii kuwaombea kwa Mungu kwa kila aliyeshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kusherehekea siku hii adhimu. Bosi wangu, Kulwa Karedia, Novacatus Makaranga, Bakari Kimwanga, Grace Hoka, Denis Luambano, Simon Regis, Hassan Bumbuli, Anthon Siame, Jonathan TiTO, Selemani Shineni, Asham Haji, Evance Magege na wafanyakazi wote wa New Habari, bila kusahau kumuombea Mungu Mhariri Mtendaji wetu, Absalom Kibanda, nikiamini kuwa Mungu ataendelea kumpigania na kurudisha afya yake ili arejee kwenye majukumu yake ya Kitaifa.

Hakika, hili ni tukio kubwa kuwahi kunitokea katika maisha yangu na naomba Mungu awe upande wangu kwa kunipa hekima, busara, utulivu na unyenyekevu, sambamba na kuwaombea amani Watanzania wote.

KAJUNASON BLOG

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment