Wednesday, 6 March 2013

VIJIMAMBO: KING MAJUTO AFICHUA SIRI ZA KUANGUKA KWA FILAMU ZA VICHEKESHO

VIJIMAMBO
KING MAJUTO AFICHUA SIRI ZA KUANGUKA KWA FILAMU ZA VICHEKESHO
Mar 7th 2013, 03:58

MCHEKESHAJI nguli hapa nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ameweka wazi kuwa, wasambazaji wa kazi za sanaa wamechangia kwa kiasi kikubwa kuyumba kwa soko la filamu za vichekesho.

King Majuto aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, katika mazungumzo maalum na Saluti5 juu ya maoni aliyonayo kuhusiana na maendeleo ya filamu za Komedi hapa nchini.

"Unajua, unaweza kuandaa komedi yako kwa hata zaidi ya milioni 7, lakini unapompelekea msambazaji anataka kuinunua kwa milioni 2," alisema King Majuto.

King Majuto alisema kuwa, kutokana na hilo, waandaaji wengi hivi sasa wamekuwa wakitayarisha kazi zao katika kiwango kisichokidhi, ili kuepuka gharama na hasara na matokeo yake mashabiki wanafikia hatua ya kuzipuuza na kuzikimbia kazi zao.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment