Thursday, 7 March 2013

VIJIMAMBO: MAMA SALMA AZINDUA KISIMA CHA MAJI KATIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE -MWANZA

VIJIMAMBO
thumbnail MAMA SALMA AZINDUA KISIMA CHA MAJI KATIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE -MWANZA
Mar 8th 2013, 06:51

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akifungua kitambaa na baadaye akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,kwa msaada wa kampuni ya bia ya serengeti. Kisima hicho kimegharimu shilingi milioni sabini. Kushoto kwa mama ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Paschal Mabiti na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Jaji Mark Bomani na wamwisho ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Valentino Bangi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaidiana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Valentino Bangi kumtwisha ndoo ya maji ndugu Getrude Ndaweka ambaye ni afisa muuguzi katika hospitali ya Sekou Toure wakati wa sherehe za uzinduzi wa kisima cha maji hospitalini hapo tarehe 
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikewte akimjulia hali mtoto Juma Joseph, 6 , kutoka katika kijiji cha Karumo, wilayani Sengerema aliyelazwa katika hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria`.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua koki ya maji wakati wa kuzindua rasmi kisima cha maji katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure .
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wafanyakazi na wananchi wa jiji la Mwanza waliohudhuria shaerehe ya kuzindua kisima cha maji katika hospitali ya Sekou Toure
Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikewte akiwahutubia mamia ya wafanyakazi na wananchi wa jiji la Mwanza baada ya kuzindua rasmi kisima cha maji katika hospitali ya Sekou Toure leo. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment