Thursday 7 March 2013

VIJIMAMBO: MWAKYEMBE AKUTANA NA MADUDU MENGINE BANDARINI

VIJIMAMBO
MWAKYEMBE AKUTANA NA MADUDU MENGINE BANDARINI
Mar 8th 2013, 07:35

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe 
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe amekutana na malalamiko mazito kutoka kwa Chama cha Wakala wa Forodha (TAFFA) ambao wamedai kuna wamiliki wa meli ambao pia wanafanya kazi ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa sheria za Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) ni marufuku kampuni ya wakala wa meli kuwa na leseni ya kuingiza na kupakuwa mizigo bandarini.
Akizungumza mbele ya Waziri Mwakyembe ambaye alialikwa katika mkutano uliohusisha wadau wa kampuni za ushuru wa forodha, Makamu mwenyekiti mstaafu wa Taifa, Otieno Igogo alisema, Serikali imekosa macho ya kuona baadhi ya udanganyifu unaotumiwa na baadhi ya vigogo kupitia mamlaka za hapa nchini.

Waziri Mwakyembe alidai kushtushwa na tuhuma hizo na aliagiza apewe majina ya kampuni hizo haraka ili aweze kuchukua hatua dhidi yao.

"Hatuwezi kuonekana kama tuko likizo lazima mniletee ushahidi ofisini kwangu," alisema.

kiongozi huyo mstaafu Taifa. Alibainisha katika mkutano huo kuwa , kitendo cha umiliki wa leseni mbili kwa kampuni hizo kunaweza kuruhusu mazingira yanayoshawishi vitendo vya kifisadi kufanyika kwa urahisi.

"Kampuni ya kupakuwa mizigo halafu pia inahusika na uwakala wa kupokea mizigo ya nje ya nchi na kutoa ndani ya nchi, Mheshiwa Waziri tunaomba uangalie hilo kwani pia linaondoa ushindani wa kibiashara,"alisema Igogo.

Alizitaja baadhi ya kampuni hizo kuwa ni pamoja na Swizz Port na DHL huku akiitupia lawama mamlaka ya Sumatra kwa kushindwa kuzichukulia hatua kampuni hizo.

Igogo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Walipa Kodi nchini aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria katika umiliki wa kampuni za uwakala wa meli,Mtanzania anatakiwa kuwa na asilimia 51 ya umiliki lakini mpaka sasa hakuna kampuni hata moja inayomiliki asilimia hizo.

"Mheshimiwa Waziri, Kampuni hizo wanamiliki kampuni za meli, Watanzania wameshikizwa kama kivuli tu"alisema Igogo.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment