Thursday 7 March 2013

VIJIMAMBO: TARATIBU, TANZANIA INAELEKEA KUWA NCHI YA KIMAFYA

VIJIMAMBO
thumbnail TARATIBU, TANZANIA INAELEKEA KUWA NCHI YA KIMAFYA
Mar 8th 2013, 07:05


Matukio yanayoendelea kutokea katika nchi yetu yanaonyesha pasipo shaka kuwa, iwapo Serikali haitachukua hatua za haraka na za makusudi, Tanzania itakuwa moja ya nchi zinazojulikana kwa vitendo vya kimafya. Mbali na matukio ya vurugu za kidini katika baadhi ya sehemu za nchi ambayo tayari yamedhibitiwa, sasa yamejitokeza matukio kadhaa tunayoweza kuyaita ya kimafya.

Matukio kama hayo hutokea katika nchi zisizo na serikali au zenye serikali legelege. Katika nchi hizo, hujitokeza makundi ya kihalifu yenye kufuata sheria za msituni na kujipa mamlaka ya kuunda mfumo wake wa kihalifu kama biashara ya madawa ya kulevya, wakati mwingine kwa ushirikiano na vyombo vya dola. Ushirikiano huo huyawezesha makundi hayo kupata silaha, fedha na taarifa muhimu kuhusu kinachojiri ndani ya serikali husika.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

1 comment: