Tuesday 28 May 2013

VIJIMAMBO: ADAM NDITI - NIPO TAYARI KUICHEZEA TAIFA STARS MWALIMU AKINIHITAJI KWENYE TIMU YAKE

VIJIMAMBO
thumbnail ADAM NDITI - NIPO TAYARI KUICHEZEA TAIFA STARS MWALIMU AKINIHITAJI KWENYE TIMU YAKE
May 29th 2013, 00:11

Wakati nikiwa hapa jijini London leo hii nimepata nafasi ya kukutana na kijana Adam Nditi ambaye mtanzania anayeichezea klabu ya Chelsea ya umri chini ya miaka 21.

Nditi ambaye alizaliwa Zanzibar mwaka 1994 kabla ya kujiunga na timu ya Chelsea U13 miaka kadhaa iliyopita baada ya kuhamia England na familia yake, katika siku za hivi karibuni ameibuka kuwa mjadala mkubwa suala lake la kuichezea timu ya taifa ya Tanzania. 

Siku za nyuma shirikisho la soka nchini TFF liliwahi kutoa ripoti kwamba walijaribu bila mafanikio kuweza kumpata Adam kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza lakini hawakufanikiwa - ingawa Adam Nditi mwenyewe anakanusha hakuwahi kupokea taarifa yoyote kutoka kwa TFF wala ubalozi wa Tanzania UK kuhusu suala la kuja kuichezea Tanzania. 
"Sijawahi kutafutwa wala kutumiwa mwaliko na TFF, ingawa siku zote nimekuwa tayari kwenda kuitumikia timu yangu ya Taifa kwa sababu mie bado ni mtanzania halisi kabisa."
Mzee Eric Nditi akitukaribisha chakula cha mchana mie na Ismail Sota - baada ya Interview

Kwa upande wa baba yake ya Nditi, aitwaye Eric Nditi amesema yeye kama mzazi wa mchezaji huyo hayupo tayari kumruhusu mtoto wake kuja kuitumikia Taifa stars mpaka pale taratibu zote zitakapofuatwa. "Kiukweli kabisa kama taratibu zote hazitofuatwa Adam hatokwenda Tanzania kuichezea timu ya taifa. Sitokubali mwanangu aende Tanzania kwa taarifa za magazetini, kiutaratibu ili mchezaji aitwe kwenye timu taifa inabidi benchi la ufundi la timu husika lijilidhishe na kiwango cha mchezaji na sio kumuita tu bila kumfanyia scouting, pia inabidi mchezaji atumiwe taarifa rasmi," anasema Nditi.
Nikiwa na Adam Nditi, Ismail Sota na Johnstone Malunde
Pia Eric Nditi amesikitishwa sana na taarifa kwamba mwanae hataki kuichezea timu ya taifa ya Tanzania. "Tatizo la nchi yetu siasa zipo kila mahala, bora wewe Shaffih umekuja mpaka huku kujua ukweli. Adam ni mtanzania wa kuzaliwa na kukulia kwenye nchi hiyo na yupo tayari kuichezea nchi yake ikiwa atatakiwa na mwalimu. Napenda kuona anaisadia nchi yake lakini kwa utaratibu unaoeleweka."

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment