Wednesday 29 May 2013

VIJIMAMBO: M TO THE P NAYE AMEFARIKI ASUBUHI YA LEO

VIJIMAMBO
thumbnail M TO THE P NAYE AMEFARIKI ASUBUHI YA LEO
May 30th 2013, 02:07

M To The P akiwa na Ngwea wakiwa jijini Johannesburg siku chache zilizopita

Pigo tena kwa muziki wa Bongo Fleva baada ya ripoti kusema, M To The P aliyekuwa na Mangwea jijini Johannesburg naye amefariki dunia.

Taarifa kutoka Johannesburg zinaeleza M To The P amefariki dunia baada ya kulazwa katika hospitali ya St Helen Joseph ambayo mwili wa Mangwe umehifadhiwa.

Mangwea na M To The P walisafiri pamoja hadi Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya shoo na baadaye waliendelea na maisha yao.

Lakini juzi wakati wanatarajia kurejea nyumbani, Mangwea alikutwa amefariki dunia chumbani na M To The P akiwa taabani na akakimbizwa hospitali.

"Kweli amefariki dunia, ni Yule mwenzake na Mangwea, sasa tuko kwenye pilika ya kuandaa mazishi," alisema Thomas, mmoja wa Watanzania wanaoshughulikia suala la mazishi. 

KAKA YAKE KUUFUATA MWILI SOUTH AFRIKA
Habari zilizopatikana muda huu zinasema kuwa familia ya Mangwea inajipanga kutuma ndugu kwenda Africa Kusini leo (May 29) kwaajili ya kufanya utaratibu wa kurudi na mwili wa Marehemu Albert Mangwea.
Akiongea na Bongo5 muda mfupi uliopita dada wa marehemu aitwaye Evelyn, amesema kuwa anahitajika ndugu wa marehemu asafiri kwenda Africa Kusini kwaajili ya kufanya utaratibu wa kurudi na mwili, sababu kule hawawezi kumtoa na kumsafirisha bila ndugu yake wa karibu kwenda.

Kwa Mujibu wa Evelyn familia iko katika mipango ya mwisho ya safari hiyo ambayo kaka yao mkubwa na Mangwea ndiye anayetarajia kusafiri leo hii (May 29) kwenda South Africa kuufuata mwili.

"Habari mpya ni kwamba mtu atoke hapa Tanzania aende akachukue mwili kule hawawezi kuconfirm yaani kumtoa kumsafirisha bila ndugu yake wa karibu kutoka huku, kwahiyo ndio process zinafanywa, kaka yake mkubwa ambaye ni kaka yetu atoke hapa aende South, ndio nadhani atarudi na huo mwili. Ataondoka leo hii hii muda wowote na wakati wowote, "Alisema dada wa marehemu Albert Mangwea.

Msiba wa rapper kipenzi cha wengi Ngwea uko Mbezi Beach Goigi kwa baba yake mdogo , ukishuka goigi ukiulizia kwa mzee Mangwea kwenye msiba utaelekezwa. R.I.P

CHANZO: Bongo5

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment