Tuesday 28 May 2013

VIJIMAMBO: FLAVIANA MATATA AULA TRUWORTHS AFRIKA KUSINI

VIJIMAMBO
thumbnail FLAVIANA MATATA AULA TRUWORTHS AFRIKA KUSINI
May 29th 2013, 00:05

MAMBO yamezidi kumnyookea mwanamitindo nyota wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata, baada ya kuingia mkataba wa kutangaza nguo za kampuni inayoongoza nchini Afika Kusini na Mashariki ya Kati, Truworths.
Truworths inaongoza kwa kuuza nguo za jumla na rejareja siyo Afrika Kusini tu, ambako kuna maduka ya kuuza na kusambaza zaidi ya 400 na kuwapa kibali cha kufanya biashara hiyo katika nchi 14 za Mashariki ya Kati na Afrika.
Hatua ya Flaviana kupata nafasi hiyo, imetokana na jina lake katika masuala ya maonesho mbalimbali ya mitindo katika nchi hiyo, Uingereza na Marekani ambako ndiko anafanyia kazi kwa sasa.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment