Thursday 30 May 2013

VIJIMAMBO: YANGA YAZAWADIWA SH Mil. 25 KWA KUSHINDA LIGI KUU

VIJIMAMBO
YANGA YAZAWADIWA SH Mil. 25 KWA KUSHINDA LIGI KUU
May 31st 2013, 00:17

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi ya kuipongeza Timu ya Yanga baada ya kutwaa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara,hafla hiyo imefanyika kwenye Ukumbi wa TBL Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam.Wengine pichani ni Katibu Mkuu wa Yanga,Laurance Mwalusako pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,Mussa Katabaro.
Katibu Mkuu wa Yanga,Laurance Mwalusako akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuipongeza Timu ya Yanga baada ya kutwaa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara.Kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Mil. 25 kwa Katibu Mkuu wa Yanga,Laurance Mwalusako ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwa Timu yeyote itakayo chukua ubingwa wa Ligi Kuu.Wengine pichani ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,Mussa Katabaro,Mkurugenzi wa Fedha Yanga,Denis Oundo pamoja na Geoffrey Makau.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment