Tuesday 28 May 2013

VIJIMAMBO: KILICHOMUUA MAGWER HIKI HAPA PITIA HABARI HII TULIYO IPATA KUTOKA LENZI YA MICHEZO BLOG

VIJIMAMBO
thumbnail KILICHOMUUA MAGWER HIKI HAPA PITIA HABARI HII TULIYO IPATA KUTOKA LENZI YA MICHEZO BLOG
May 28th 2013, 23:58

Taarifa ambazo Lenzi ya Michezo imezipata kutoka Afrika ya Kusini kwa HusseinOriginal ambaye yupo Pretoria, amesema Ngwear amefariki leo asubuhi kwenye gheto ambalo alikuwepo pia msanii M to The P ambaye yeye amelazwa hospitali akiwa mahtuti. 
"Tulivyokwenda kuwagongea asubuhi tuliwakuta Ngwear amefariki na M To The P akiwa amepoteza Fahamu Kabisa"
Baada ya kuwapeleka hospitali Daktari alitibitisha amekufa na ameshatoa taarifa kwa watu wa Karibu wa Ngwear huko Afrika nya Kusini.


Ngwea akiwa na msanii M to the P walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezimia kwenye chumba wote wawili baada ya kuzidisha (overdose) madawa ya kulevya na M to the P.


Hata hivyo mama yake Ngwear ambaye yupo nyumbani kwao Morogoro amethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanae na kusema kuwa taarifa za kuwa za kuwa alikuwa Afika ya Kusini alikuwa hana kwani mara ya mwisho kuongea naye zimepita wiki mbili sasa.


Pia amesema taratibu za maandalizi ya mazishi yatakavyokuwa yataanza baada ya kufika baba yake mdogo Ngwear ambaye yupo mkoani Ruvuma kwani anatarajiwa kuwasili kesho Morogoro.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment