Wanamasumbwi leo kwa uchache walijikusanya katika viwanja vya leaders na kukipiga mechi ya kirafiki ya kudumisha uhusiano mzuri baina yao. mechi hiyo ambayo iliandaliwa kimzaha huku baadhia ya wanamasumbwi wakiwa hawana taarifa ya mchezo huo walikurupuana asubuhi na kucheza mechi hiyo bila wasiwasi kana kwamba mpira wanaujua. walikuwa waandishi ndio walioanza kuliona lango la mabondia dakika za mwanzo za mchezo kupitia kwa majuto omar aliyepiga shuti kali la mbali ambalo lilimshinda bondia chipukizi issa omar na kuwa goli,huku wakicheza bila kujitambua mabondia walionesha uhai pale alipotoka paquiao na kuingia jose mbowe ambae aliwasumbua kimpira na kufunga goli kwa upande wa mabondia.
kipindi cha pili timu zote zilijipanga vizuri na hazikuweza kufungana huku mpira ukiiisha mabondia wakiwa bado apo fiti wakihitaji kuendelea na waandishi wakionekana wapo hoi kwa mikiki ya uwanjani.timu hizo zimepanga yafanyike marudiano zote zikiwa kamili.YAWEZA KUWA MECHI YA KUCHANGIA KITUO CHA MICHEZO YA NDANI (indoor)
Alphonce mchumia tumbo akiwa chini ya ulinzi wa mabaki wa taswa.
Francis Miyeyusho anajiandaa kutoka na nafasi yake ikachukuliwa na mashali.
ibrahim'bigright akitoa maelezo kwa timu ya mabondia huku thomas mashali akisikiliza kwa makini kabla ya kuingia.
majuto omari wa taswa na jimwili lake kashindwa kabisa kufurukuta kwa daudi muhunzi.majuto ndie aliefunga bao la pili la taswa.hapa kabla hajatulizwa kibondia.
Juu na chini ni timu ya mabondia ikipata mawaiza.
No comments:
Post a Comment