Saturday 18 May 2013

VIJIMAMBO: MBUNGE AANGUKA BUNGENI LEO

VIJIMAMBO
thumbnail MBUNGE AANGUKA BUNGENI LEO
May 18th 2013, 21:08

MBUNGE wa Viti Maalum, pichani Mwanamrisho Taratibu Abama (Chadema), ameanguka bungeni, baada ya kujisikia vibaya.

Mbunge huyo alianza kujisikia vibaya, hali iliyomfanya kuketi katika viti vilivyo karibu na zahanati ya Bunge.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia walisema mbunge huyo alipata huduma ya kwanza katika zahanati hiyo kwa zaidi ya saa mbili kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Dodoma.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya hospitali hiyo, zinasema mbunge huyo alilazwa wodi namba 18.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Zainab Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mbunge huyo.

"Ni kweli yupo hapa na hali yake inaendelea vizuri sasa ,"alisema.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment