Friday 10 May 2013

VIJIMAMBO: WANANCHI KUANZA KUSAFIRI KUTOKA MTWARA HADI BUKOBA KWA LAMI

VIJIMAMBO
thumbnail WANANCHI KUANZA KUSAFIRI KUTOKA MTWARA HADI BUKOBA KWA LAMI
May 11th 2013, 01:09


Na Immaculate Makilika- Dodoma
WANANCHI wataweza kusafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwenye barabara ya lami.
Hayo yamesemwa leo hapa Bungeni mjini Dodoma wakati Waziri wa Ujenzi John Magufuli alipokuwa akijibu swali la Martha Mlata(Viti Maalum-CCM), lililohoji juu ya ahadi ya Serikali katika kipindi cha Awamu ya Nne na iliyosema wananchi wataweza kusafiri kwa taxi toka Mtwara hadi Bukoba.
,J e utekelezaji wa ahadi hiyo umefikia wapi.
Aidha Waziri Magufuli alisema kuwa nia ya msemo huo ni kuonesha kwamba wananchi wataweza kusafiri toka Mtwara hadi Bukoba kwa lami na kuongeza kuwa lengo hilo limetekelezwa kwa mafanikIo makubwa hadi kufikia asilimia 99 ya barabara yote kutokea Mtwara hadi Bukoba.


Hata hivyo Magufuli aliendelea kwa kwa kusema kwamba barabara yote kuanzia Mtwara - Dar es Salaam- Dodoma-Singida- Nzega-Tinde-Usagara pamoja na Geita-Bwanga-Kyamyorwa hadi Bukoba yenye urefu wa kilometa zipatazo 1,989 imejengwa kwa kiwango cha lami.


Isipokuwa sehemu fupi yenye urefu wa takribani kilometa 26 katika barabara ya Ndundu-Somanja ambayo itakamilika kujengwa kwa kiwang o cha lami kabla ya Desemba,2013.


Alisema Serikali ya awamu hiyo itahakikisha ahadi ya wananchi kusafiri kwenye barabara ya lami toka Mtwara hadi Bukoba inatekelezwa.

You are receiving this email because you subscribed to this feed at blogtrottr.com.

If you no longer wish to receive these emails, you can unsubscribe from this feed, or manage all your subscriptions

No comments:

Post a Comment